Na Thadei Hafigwa
WANANCHI wa
Jimbo la Morogoro Kusini wameanisha kero na kuziwasilisha kwa Mgombea ubunge
kwa tiketi cha chama cha Mapinduzi,Zuberi Mfaume ili zipatiwe ufumbuzi ikiwemo
changamoto za miundombinu ya barabara,maji, uchungaji holela wa mifugo
ilinayoharibu mazao ya wakulima shambani husuan kipindi cha kilimo.
Wakazi wa Kata ya
Selembala,Kisaki,Mvuha,Mngazi na Bwakila chini Morogoro vijijini wamebainisha
hayo kwa nyakati tofauti kwenye mikutano kampeni inayoendelea jimboni humo
ambapo wameonesha imani walionayo Mgombea ubunge wa ccm jimbo la Morogoro
kusinijambo lililowalazimu wagombea wengine kutoka vyama vingine vya kisiasa
walionesha nia ya kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo hilo kutorudisha fomu walizochukua tume huru ya
taifa ya uchaguzi.
Zuberi Mfaume ni Mgombea pekee ubunge Jimbo la Morogoro kusini kwa tiketi ya CCM ambaye Oktoba 29, 2025 siku ya Kupiga kura atapigia kura ya Ndiyo au Hapana kwenye kinyang’anyiro hicho.
Wagombea nafasi ya udiwani na Mgombea Ubunge,Jimbo la Morogoro Kusini,Zuberi Mfaume wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya viongozi wa ccm wilaya ya Morogoro vijijini,mara baada ya kumaliza harakati za kunadi Ilani ya CCMMfaume akiwa katika
mikutano yake ya kampeni katika kata ya Selembala,Mvuha,Kisaki,Mngazi na
Bwakila Juu, amejitwika mzigo wa changamoto zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo ambazo ni miundombinu ya
barabara,uchungaji holela wa mifugo ambayo inaharibu mazao ya wakulima,stakabadhi
ghalani pamoja na pungufu wa maji katika maeneo ya vijijini ambayo kwa mujibu
wa sera ya maji,inayoelekeza wakazi wa vijijini wanapaswa kufikiwa huduma ya usambazaji
wa maji kwa asilimia 85.
amewahakikishia wananchi wa
maeneo hayo kuwa changamoto zinazowakabili zitashughulikiwa mara baada ya kuchaguliwa kuhudumu nafasi ya ubunge
kwa kuwa tayari ashaandaa mkakati maalum wa kuzipatia ufumbuzi changamoto zilinazowakabili
wananchi,.
“kipaumbele changu cha
kwanza nitaimarisha ofisi ya mbunge kwa kuweka dawati la msaada wa sheria ili kuwasaidia
wananchi kukabiliana na changamoto za kisheria”alisema.
Mgombea huyo mbali na
taaluma nyingine alizonazo pia ni mwanasheria, alinukuu ahadi iliyoanishwa
kwenye Ilani ya CCM 2025-2030 iliyoelezea utatuaji wa changamoto ya miundombinu
ya barabara kutoka ubenazomozi hadi Mvuha.
“ahadi namba 265 katika Kitabu cha Ilani ya chama cha Mapinduzi unasomeka Mradi wa upembuzi yakinifu katika barabara ya Ubenazomozi, Ngerengere, kuelekea kituo cha SGR,Tununguo,Selembala,Mvuha inaungana na Bigwa Kisaki kuelekea bwawa la Mwalimu Nyerere itajengwa katika kiwango cha lami”.
“pamoja kutambua sheria
hiyo ya ardhi na vijiji katika kutatua changamoto za migogoro ya ardhi inapaswa
wanakijiji kuunda sheria ndogondogo na kutambua Sheria ya serikali za
Mitaa,Mamlaka ya Wilaya,Sura 287 toleo la mwaka 2023,kwamba kifungu cha 170 kinaeleza Mamlaka ya serikali ya
Kijiji kutunga sheria zake,village by laws”alisema.
Alibainisha ya kuwa,Kata ya
Selembala imeingizwa katika barabara kuu inayotoka Ubenazomozi mpaka Mvuha ambayo tayari imeingizwa katika
upembuzi yakinifu ili ijengwe kwa kiwango cha rami,kwamba imetafsiriwa kama
barabara kuu kuelekea katika bwawa kubwa la kufufua umeme,Bwawa la Nyerere.
Pia, Mgombea Ubunge Jimbo
la Morogoro Kusini ameahidi kushughulikia changamoto ya miundombinu ya barabara
kutoka eneo la getini hadi Kijiji cha Kiganila kilichopo kata Selembala kwa
kutumia mfuko wa jimbo.
“ninataka kuwaahidi kwamba
serikali ya Chama Cha Mapinduzi ilitenga fedha maalum ya mfuko wa jimbo,moja ya
kazi zake ni kutatua changamoto kama hizi,nitakuja kuwashukuru,tutakaa pamoja
na tutaona namna gani tutapitisha greda walau barabara yetu iweze
kupitika”alisema.
Aidha,alianisha changamoto
nyingine ni changamoto ya vijiji viwili Bwilachini na Kibulumo vilipitiwa na
mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere toka mwaka 2019 wananchi wa vijiji hivyo hawana
uongozi baada ya kupatiwa eneo lingine la kuishi, la mjipya.
Mzee Zuberi Mwenegoha diwani
mstaafu wa Kata ya Selembala anasema kwa sasa wananchi wanasubiri maelekezo ya
uongozi wa CCM Mkoa wa Morogoro ambao wameahidi kulishughulikia suala hilo.
“kwa sasa tunasubiri
uongozi wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Morogoro ambao wameahidi kuja
kututembelea na kusikiliza kero zetu ili zipatiwe ufumbuzi kwa kuwa ndicho
chama chenye dola”alisema Mzee Mwenegoha.
Katika mikutano yake
amekuwa alitoa elimu ya sheria umuhimu wa kuishi bila ya kubaguana kati ya
wakulima na wafugaji akinukuu katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.ibara
ya 13(1).
“Watu wote ni sawa mbele ya
sheria, na wanayo haki,bila ya ubaguzi wowote,kulindwa na kupata haki awa mbele
ya sheria.”
Hoja hiyo imekuja baada ya
wananchi kuelezea kero walionayo ya mifugo kuingia kwenye mashamba ya wakulima
na kuharibu mazao. “Mkulima hana haki ya kuugua mifugo ya wafugaji,wala mfugaji
hana haki ya kuingiza mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu
mazao.”alisema.
Aliwaahidi wananchi
kumwamini kero zinazowatatiza zitawekewa utaratibu maalum wa kuzishughulikia sanjaria
na kuzingatia sheria za nchi bila ya kumuonea mtu yeyote.
Temotheo Tapo kutoka jamii
ya wafugaji mkazi wa Kijiji cha Mgogoni,Kata
ya Selembala amesema baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba ya watu
na kuharibu mazao si jambo jema,hata hivyo aliomba serikali kuhakikisha
wanawawekea mazingira mazuri ya kujengea malambo yakunyweshea mifugo.
“Mifugo yetu inakosa
maji,serikali imetukataza kutumia maji ya mito kunyweshea mifugo yetu.mifugo
yetu pia inakabiliwa na magonjwa ya mapafu,midomo na miguu kuvimba tunahitaji
majosho”alisema Tapo.
Katika ziara ya Kampeni Zuberi alimbatana na viongozi mbalimbali wa chama,Katibu wa Vijana wa Wilaya ya Morogoro vijijini,Mussa Idowa,wajumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Morogoro vijijini, Donny Mbena,Zamoyoni Zuberi, Scolastika Salum,Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Morogoro, na Hamza Yahya mjumbe wa halmashauri kuu CCM Mkoa wa Morogoro.
Kwa
nyakati tofauti walinadi wagombea kwenye mikutano ya kampeni ili kuhakikisha
wananchi wanajitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na wanachagua wagombea wanaotokana
na chama cha mapinduzi,Samia Suluhu Hassan katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Zuberi Mfaume nafasi ya ubunge pamoja na madiwani
wanaogombea katika kata 17 zilizopo kwenye Jimbo la Morogoro kusini.
Kwa upande wake Mjumbe wa
halmashauri kuu ccm Mkoa wa Morogoro,Hamza Yahya aliwahimiza wanachama na
wapenzi wa chama hicho kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wengine wenye sifa
ya kupiga kura wanajitokeza na kukipigia kura chama cha mapinduzi ili falsafa
ya mafiga matatu iweze kutekelezeka kwa vitendo,kwa kuzingatia mnyororo wa
uwajibikaji wa pamoja.
Jimbo la Morogoro kusini lina
jumla ya kata 17 ambazo ni Mtombozi,Selembala,Bungu,Mvuha,Kisemo,Kasanga,Konde,Lundi,Kibuko,Kolero,Tawa,Kibogwa,Bwakira
chini,Kisaki,Mngazi, Bwakila juu na Singisa.


.jpg)

No comments:
Post a Comment