Breaking News

Dec 21, 2020

DC KILOSA ATAKA MADIWANI KUWASIMAMIA WENYEVITI WA VIJIJI KUWAJIBIKA

  

MKUU WA WILAYA YA KILOSA,ADAM MGOYI,AKIWAHUTUBIA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA

DC  KILOSA ATAKA MADIWANI KUWASIMAMIA WENYEVITI WA VIJIJI 

   Na Thadei Hafigwa                               

 MKUU wa Wilaya ya Kilosa,Adam Mgoyi amesema wenyekiti wa vijiji wasio wajibika kwa wananchi katika kuitisha vikao vya kikanuni kwa kipindi vitatu mfululizo wataondolewa kwenye nyadhifa zao  ili kero za wananchi ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka. 

Mgoyi amesema kwamba, kutokana na viongozi wengi wamechaguliwa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) hataruhusu kuona chama hicho kinadharirika kutokana na uzembe unaofanywa na baadhi ya viongozi.

Mkuu wa Wilaya alitoa rai hiyo, kwa madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Desemba 18,2020 katika hafla ya kiapo kwa madiwani baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 na kuongeza kuwa madiwani wanawajibu wa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa katika uendeshaji wa halmashauri.

“Wilaya yetu inakabiliwa na malalamiko mengi lakini yote inatokana na suala ya utawala bora,katika vikao vya kisheria katika kipindi cha miaka 5 iliyopita katika vijiji 138 ni asilimia 20 pekee ndio walitimiza wajibu wao.”

Pia, wananchi wanahitaji kuongezewa uelewa katika utendaji kazi wa serikali,lakini badala madiwani kuwasaidia wananchi katika maeneo yao, lakini mnaongozana nao hadi ofisi ya mkuu wilaya”Alisema DC Mgoyi

Aidha, aliwaasa madiwani kujielekeza zaidi katika kushughulikia kero za wananchi katika ngazi vijiji badala ya kutegemea zaidi wananchi kukimbilia ofisi ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri kwani kwa kufanya hivyo kutambukiza foleni za wananchi kuelekea ofisi ya mkuu wa Wilaya.

MKURUGENZI MTENDAJI,HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA,ASAJILE MWAMBAMBALE AKITOA NASAHA KWA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA,MKOA WA MOROGORO.

Asajile Mwambambale ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kilosa katika hafla hiyo,aliahidi kutoa ushirikiano kwa madiwani wote,katika kutatua changamoto zilizopo wilayani humo ili wananchi waweze kupata maendeleo.

Mwambambale alisema kuwa ofisi yake ipo wazi katika kuhakikisha malengo waliokuwa nayo madiwani wa kuleta maendeleo kwa wananchi yanafanikiwa na kusimamiwa kikamilifu.

HAKIMU MKAZI WILAYA YA KILOSA,FELISTA GILBERT AKIWAONGOZA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA KIAPO CHAO

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya kilosa waliapa mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Kilosa,Felista Gilbert ambapo baada ya kiapo hicho,Hakimu huyo aliwasa madiwani kuzingatia kiapo chao kutokana na dhamana waliopewa ya kuwahudumia wananchi.

Katika hatua nyingine, madiwani walichagua mwenyekiti wa halmashauri,makamu wake pamoja na viongozi wa kamati 3 za kudumu ambapo katika uchaguzi wao ulisimamiwa na katibu tawala wa Wilaya ya Kilosa,Yohana Kasitila.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA,MKOA WA MOROGORO,WILFRED SUMARI AKISISITIZA JAMBO.
Katibu tawala wa wilaya, kwa kuzangatia kanuni za uendeshaji wa halmashauri, ndiye mwenyekiti wa kusimamia mchakato wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya na makamu wake,ambapo baada ya madiwani kupiga kura walimchagua Wilfred Sumari kuwa mwenyekiti wa halmashari  ya Kilosa na vicenti Elias kuwa makamu wa Mwenyekiti kwa kuchaguliwa kwa asimilia mia moja.

KATIBU TAWALA WILAYA YA KILOSA,YOHANA KASITILA AMBAYE AKIENDESHA KIKAO CHA UCHAGUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOSA.


Hafla hiyo imehudhuriwa na Mbunge wa Kilosa kati,pia Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi,Mbunge wa Mikumi Dennis Londo,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilosa,Ameir Mbarak na wadau mbalimbali wa maendeleo.
WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI(KULIA) AKITETA JAMBO NA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KILOSA,AMEIR MBARAK KUSHOTO,HUKU MBUNGE WA JIMBO LA MIKUMI DENNIS LONDO KATIKATI AKIFURAHIA MAZUNGUMZO HAYO.
 

No comments:

Post a Comment