Breaking News

Dec 22, 2024

'MSOUTH 'Atoa Zawadi ya Mavazi kwa Wazee 110 Kingolwira


Valentino Nyefwe (msouth)kushoto akimkabidhi  Diwani wa Kata ya Kingolwira Madaraka Bidyanguze mfuko uliohifadhia msaada wa nguo kwa ajili ya wazee wa Kata hiyo. 

Na Thadei Hafigwa

WAZEE wa Kata ya Kingolwira, Manispaa ya Morogoro wamejikuta wakibugujikwa na machozi ya furaha baada ya kupokea msaada wa mavazi ya aina mbalimbali kutoka familia ya Valentino Khan Nyefwe (msouth).

Katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa nguo ulitolewa na familia ya msouth

Diwani wa Kata ya Kingolwira,Madaraka Bidyanguze  amesema kuwa wazee wa Kata yake ni watu wenye tabia njema,wenye busara na wenye moyo wa shukran  pia ni wacha mungu.

Katibu wa Baraza la wazee Kata ya Kingolwira, Scolastica Mluge (kulia) aliyevaa vazi la rangi ya bluu akiendesha zoezi la kugawa nguo kwa wazee.Katikati ni mdau wa maendeleo Valentino Nyefwe akishuhudia zoezi hilo.

Bidyanguze akitoa shukran kwa niaba ya wazee wa Kingolwira amesema ofisi ya Kata inatambua mchango wa hali na mali inayotolewa na msouth kama mdau wa maendeleo katika kusukuma maendeleo mbalimbali ya wananchi.

Alisema kuwa msouth wakati mwingi amekuwa na moyo wa aina yake kwa kuonesha utayari nyakati zote bila ya kuchoka.

Baadhi ya wazee walioshiriki katika hafla ya utoaji wa Zawadi ya Mavazi kwao iloyotolewa na mdau wa maendeleo,Msouth(Valentino Nyefwe)

Valentino Nyefwe alikingozana na familia yake walitoa msaada wa nguo kwa wazee wa Kata ya Kingolwira 110,ambapo Uongozi wa Baraza la Kata ya Kingolwira,Scolastica Mluge na msaidizi wake Iddi kamandwa uliratibu wa kuhakiki wazee kwa kuwashirikisha viongozi  wa serikali za mitaa 8 iliopo kwenye Kata hiyo.

Sehemu ya familia ya mdau wa maendeleo,msouth(Valentino Nyefwe) walusaidia zoezi la Ugawaji wa Zawadi ya nguo kwa wazee wa Kingolwira)

Katibu wa wazee Scolastica Mluge alitaja mitaa hiyo ni Shule,zahanati, tambukareli,seminari,tenki la maji na mtaa wa mahakamani.

Kwa upande wake msouth alisema yeye na familia yake wamewiwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Kingolwira kupitia ofisi ya diwani.

Diwani wa Kata ya Kingolwira, Madaraka Bidyanguze akizungumza kwenye hafla ya Ugawaji wa Zawadi ya nguo kwa wazee wa Kingolwira 

Alisema kuwa,mara kwa mara amekuwa akiguswa na kuwapwnda wazee kwa kuwa wakati wakiwa na nguvu walimwaga jasho lako katika ujenzi wa Taifa hivyo kwa kuwa wameishiwa nguvu wanapaswa kusaidiwa kwa hali zote ikiwemo mavazi,makazi,chakula na matibabu.

Wazee wa Kingolwira walioshiriki kwenye hafla ya utoaji wa Zawadi ya nguo

"baadhi yenu tumewasaidia katika kupata bima ya afya pamoja na makazi,kwa mtazamo wangu nimeona ni jambo jema nilipochukua uamuzi wa kumjengea nyumba Mzee mmoja ili aweze kupata mahali pa kuishi badala ya kumpa fedha."alisema.

Alisema kuwa ataendelea kuwasaidia kwa kadri mungu atakavyomjalia,huku akionesha utayari wake wa kukubali kuwa mlezi wa wazee baada ya kuombwa na Uongozi wa Baraza hilo la wazee Kata Kingolwira.

No comments:

Post a Comment