Uongozi wa chama Cha Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro (MoroPC) umetoa pongezi kwa Mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi na watumishi wa umma(PSSSF) kwa kuandaa Fursa ya mafunzo kwa Waandishi wa Habari mjini hapa.
Mwenyekiti wa MoroPC,Nickson Mkilanya alibainisha hayo Desemba 14,2024 katika mafunzo kwa Waandishi wa Habari ambao ni wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro.
Nickson Mkilanya, mwenyekiti MoroPC akieleza umuhimu wa mafunzo hayo.Mkilanya alisema kuwa Waandishi wa Habari wa Morogoro wapo tayari kushiriana na PSSSF katika kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari juu ya huduma zinazopatikana na kutolewa na mfuko huo nchini.
Alisema kuwa PSSSF isihofu kufanyakazi na mwandishi wa Habari yeyote aliopo mkoani Morogoro Lakini itakuwa vizuri shughuli hizo zikapitia kwenye Klabu ya Waandishi wa Habari ili kuleta tija na ufanisi.
Waandishi wa Habari mjini Morogoro Wakishiriki katika mafunzo.mmoja wa Waandishi wa Habari wakongwe,ambaye pia ni mnufaika na mfuko huo, Bujaga Izengo Kadago alitoa ushuhuda juu ya huduma bora ya utoaji wa mafao ya kuustaafu inayotolewa na mfuko huo.
Bujaga amesema kuwa baada ya kuustaafu kwake katika utumishi wa umma alifuatilia mafao yake, kwa mterezo bila ya kuwepo na vikwazo ambapo mafao yanatolewa kwa wakati.
Kwa upande wake,Meneja wa mawasiliano na utoaji elimu kwa umma PSSSF,Yesaya mwakifulefule alisema kwa sasa Wana mkakati wa kuelimisha umma kwa kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari Nchini kupitia Klabu za Waandishi wa Habari mikoani ili kupanua Wigo wa uwelewa kwa jamii na umma.
Meneja wa mawasiliano na utoaji Elimu kwa umma,Yesaya mwakifulefule alisisitiza jambo katika mafunzo kwa Waandishi wa Habari,mjini Morogoro.Pia,Waandishi wa Habari katika mafunzo hayo walipata fursa ya kukuuliza maswali jinsi ya mfuko huo ulivyojipanga katika mfumo wa kidigiti kwa wanachama wake waliopo vijijini ambao wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya tehama
Mwakifulefule alisema mfumo huo umejipanga vizuri na changamoto ya tehama ambayo hapo awali ilikuwa ikiwasimu wanachama wa mfuko huo,lakini kwa sasa kero hiyo imekupungua na wanachama wanaridhishwa na huduma.
Picha ya pamoja iliyowashirikisha Waandishi wa Habari na maafisa wa PSSSF mara baada ya. Mafunzo.Alisema kuwa mafunzo hayo ni endelevu yanaendelea kutolewa ili kuyafikia makundi yote bila ya kumwacha mtu yeyote nyuma katika falsafa ya PSSSF kiganjani ia yatatolewa kwa awamu kwa kadri ya mahitaji na utekelezaji wa mpango mkakati wa utoaji elimu kwa umma juu ya mfuko huo.
No comments:
Post a Comment