Na Thadei Hafigwa Morogoro
SERIKALI imesema kuwa kupitia wizara ya elimu sayansi na teknolojia inajitahidi kuhakikisha inatoa elimu inayotolewa sasa inaendena na mabadiliko ya teknolojia duniani ili kurahisisha maendeleo nchini bila ya kuachwa nyuma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Daniel Mushi alisema hayo wakati akifungua Kongamano la Kimataifa la Taaluma ya Maendeleo linalohusisha Vyuo Vikuu vya ndani na Nje ya Nchi linalofanyika mjini Morogoro.
Profesa Mushi alisema kuwa iwapo teknolojia ikitumika vibaya inaweza kuiharibu jamii,pia ikitumika vizuri inaweza kuinufaisha jamii,kwamba njia sahihi ni wananchi kuelimishwa na kushirikishwa dhana sahihi ya maendeleo kupitia wataalam.
“Maendeleo ya nchi hayapatikani bila kuwepo na ushirikishwaji,serikali ina kushirikiana na sekta binafsi,wadau wa maendeleo kwa kuunda utatu wa maendeleo” alisema.
Alisema kuwa katika ushirikiano huo kila upande unapaswa kuwa na dhana sahihi ya maendeleo ambapo kongamano la Morogoro ni kujengeana uelewa sahihi wa kuweza kushirikishana katika utatu wa kuleta maendeleo.Washiriki wa Kongamano la kimataifa wakifuatilia hoja kutoka kwa watoa mada mbalimbali
Alisema kuwa katika kongamano hilo litakuwa na majawabu ya namna bora ya kuweza kuwafundisha wanafunzi vyuoni ili aweze kuwa na mtazamo sahihi wa dhana maendeleo.
Alisema kuwa dhana ya maendeleo inabadilika kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia,ikiwemo akiliumba(mnemba) katika kujifunza namna ya kutofautisha kazi iliyoandikwa na mwanafunzi kwa kutumia uwelewa wake na utashi wake na ailiyopita kupitia akiliumba.
Kwa upande wake,Profesa William Mwegoha, Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe(MU) alisema Kongamano hilo linaangalia mfumo na muktadha wa taaluma za maendeleo katika ulimwengu unaoendelea kubadilika katika kiazazi cha sasa na kijacho ili kuleta matokeo chanya.
Profesa Mwegoha alisema kuwa mkutano huo umebeba lengo la kuangalia taaluma za kimaendeleo katika ulimwengu wa mabadiliko ,ikiwemo teknolojia,uchumi na changamoto mbalimbali ,mabadiliko ya tabianchi sanjali na kufanya mapitio katika taaluma za maendeleo zipitiwe ili ziendelee kuwa na thamanika.
Profesa Elizabeth Lulu Genda ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Maendeleo chuo kikuu Mzumbe, ,alibainisha kwamba ni kongamano hilo ni la tatu la kimataifa limekuwa na mijadala ya kujadili maendeleo kwa kadri ya nyakati na mwaka husika.
Kongamano hilo la Kimataifa limeandaliwa kwa ushirikiano wa Vyuo Vikuu vitano,ikiwemo Chuo kIkuu Mzumbe,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,(UDSM),Chuo kikuu Dodoma,Chuo Kikuu cha Afya(MUHAS) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) ikiwa na mada 70 zinazotolewa na wataalamu mbalimbali ndani na nje ya nchi likiwa na kauli mbinu isemayo,mtazamo wa kitafiti wa Maendeleo kwa kizazi cha sasa na kijacho.
No comments:
Post a Comment