BAADHI YA WAUMINI WA KANISA KATOLIKI WAKIWA WAMEVAA BARAKOA IKIWA NI SEHEMU YA MAPAMBANO DHIDI YA COVID 19
KANISA KATOLIKI YAHADHARISHA WAUMINI DHIDI YA CORONA
Na angel Mbwana
KANISA Katoliki
limeendelea na hatua ya kuwahadharisha waumini wake dhidi ya corona kwa waumini
kunawa mikono kwa maji tiririka kabla ya kuanza ibada huku liturjia ya ekaristi
ikiendesha kwa umakini mkubwa.
Wakati wote Kanisa Katoliki,halijatetereka kuwahimiza waumini wake kuchukua tahadhali kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya mapafu (covid 19) unaosumbua duniani ambapo wakati wa kukomunika waumini wanahitajika kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kusimama wa mita chache kabla ya kukomunika.
Baadhi ya waumini waliohojiwa na Mwandishi wa habari hizi,Rosemary Kobero amesema kuwa wanaishukuru serikali pamoja na kanisa kushirikiana katika utoaji wa elimu ya kujikinga na covid 19 ili kuepuka maambukizi mapya.
Hivi karibuni Baraza la Maaskofu Tanzania(TEC) na taasisi nyingine za dini ikiwemo Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) ziliandaa waraka wenye ujumbe wa kuchukua tahadhari za kiafya kwa waumini wao ikiwa ni moja ya hatua ya kuunga mkono harakati za mapambano dhidi ya covid 19.
Miongoni mwa tahadhari
hizo ni uvaaji wa barakoa,unawaji wa mikono kwa maji tiririka,kukaa mbali kiasi
toka kwa wengine,kufunika kinywa(mdomo) wakati wa kikohozi au kupiga chafya kwa
kiwiko cha mkono,tishu au leso.
Kadhalika kunizingatia maagizo na maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu wa afya katika kukabiliana na maambukizi ya covid 19.
No comments:
Post a Comment