Breaking News

Feb 4, 2021

JUMUIYA WAZAZI MOROGORO AHAMASISHA UPANDAJI MITI

 


JUMUIYA WAZAZI MOROGORO AHAMASISHA UPANDAJI MITI

Na Severin Blasio,Kilosa

 

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa Morogoro, Heri Hoza amezitaka shule binafsi na za serikali kupanda miti ya mbalimbali kwenye maeneo ya shule ili kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 44 ya Chama cha Mapinduzi CCM, yaliyofanyika kijumuiya katika shule ya sekondari Mkono wa Mara wilayani Kilosa,  Hoza alisema kuwa, suala la kutunza mazingira ni muhimu kutokana na kipindi hiki misitu mingi kukatwa kwa matumizi mbalimbali ya nishati na ujenzi na hivyo kusababisha mabadiliko ya tabia nchi.

“Suala la upandaji miti katika shule za serikali na za binafsi haliwezi kuepukika,kutokana na uharibifu mkubwa wa misitu katika mkoa wetu.hivyo naagiza upandaji miti kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi”alisema Hoza.

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA MOROGORO,HERI HOZA AKIPANGA MTI

Aidha, Mwenyekiti Hoza, aliwataka wananchi wote kuiga mfano wa upandaji miti ikiwa ni hatua ya kurudisha miti ambayo iliyotumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na nishati kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji ambavyo vianaweza kutoweka.

Aliwataka viongozi wa chama  na jumuiya ya wazazi kuanzia tawi na wilaya ya Kilosa kuhakikisha wanafika shuleni hapo mara kwa mara kukagua maendeleo ya shule hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri endapo kutajitokeza changamoto katika shule hiyo.

Pia, aliwataka wadau mbalimbali wakiwemo wanachama kutoa msaada kwa ajili ya kupunguza changamoto ya majengo na samani katika sekondarihiyo.

Awali akitoa taarifa ya sekondari ya mkono wa mara mkuu wa shule Samwel Swai alisema shule hiyo inachangamoto lukuki ikiwemo uchakavu wa majengo na samani hivyo kuomba msaada kwa chama kusaidia kumaliza changamoto hiyo

Hata hivyo, Swai alisema kuwa, kwa kutumia miti iliyopo hapo shuleni wamechonga madawati zaidi ya 70, hivyo angalau kupunguza uhaba wa samani katika shule hiyo.

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI MKOA WA MOROGORO,HERI HOZA AKIKAGUA MADAWATI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MKONO WA MARA,WILAYA YA KILOSA(PICHA NA SEVERIN BLASIO)

Maadhimimisho hayo yaliambatana na shughuli za kupanda miti ambapo jumla ya miti mbalimbali ikiwemo ya mbao na matunda 92 ilipandwa katika sekondari ya Mkono wa mara ambayo inamilikiwa na Jumuiya ya wazazi.

No comments:

Post a Comment