Breaking News

Sep 25, 2024

BENKI NMB YAPONGEZWA KUDHAMINI MASHINDANO YA SHIMIWI

 

BENKI NMB YAPONGEZWA KUDHAMINI  MASHINDANO YA SHIMIWI

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

BENKI ya NMB impongezwa kwa kuwa mdhamini kuu wa michezo ya shirikisho la michezo ya Wizara na Idara ya Serikali kwa kipindi cha miaka Mitatu mfululizo.

Hayo yameelezwa Septemba 25,2024 na Mwenyekiti wa SHIMIWI,Daniel Mwalusamba katika taarifa yake aliyoitoa kwenye hafla ya ufunguzi wa michezo hiyo katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro ambayo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Doto Mashaka Buteko,ambaye alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.


Meneja Mwandamizi Benki ya NMB huduma za kibenki na mahusiano kwa serikali,Amanda Feruzi aliongea na waandishi wa Habari,muda mfupi baada ya mashindano hayo kufunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Doto Mashaka Buteko

Mwalusamba alisema kuwa Benki ya NMB imekuwa mdau Mkubwa wa michezo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Sita,inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan.

Brass band ya Jeshi la Magereza liliongoza maandamano ya wanamichezo kutoka Wizara,Taasisi na Idara za serikali 

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi Benki ya NMB huduma za kibenki na mahusiano kwa serikali,Amanda Feruzi amesema kuwa katika mashindano hayo wametoa jezi, bukta,trakisuti,viatu vya michezo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali.

Feruzi alisema kuwa benki ya NMB kwa  kipindi cha takribani miaka mitatu mfululizo benki ya NMB imekuwa ikishirikiana na shimiwi katika kuendeleza michezo kwa kwa kutoa vifaa vya michezo,hivyo wameonesha furaha katika kushiriki katika mashindano hayo kwa mwaka 2024.

Baadhi ya wanamichezo wakiwa wameshika mabango wakiingia ndani ya uwanja wa Jamhuri wakati wa ufunguzi wa Shimiwi,uwaja wa Jamhuri Mjini Morogoro

amesema kuwa mahusiano yaliopo baina ya taasisi hiyo ya fedha na serikali hayaishi tu kwenye shughuli za kibiashara bali pia kwenye michezo ikiwa ni  mikakati yake ya kuendeleza michezo na kuwasogezea huduma wananchi na  wateja wake huduma zinazotolewa na benki hiyo.

Alisema kuwa katika mbali na huduma hiyo ya kutoa vifaa vya michezo pia wanawahudumia wananchi waliotembelea katika banda la NMB lililopo katika uwanja wa Jamhuri ambako mashindano hayo yanafanyika.

Kabla ya ufunguzi wa mashindano hayo,Klabu 57 kutoka Wizara na Taasisi za serikali ziliingia uwanjani kwa maandamano na kupokelewa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Doto Mashaka Buteko.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni,Naibu Waziri wa sanaa,utamaduni na Michezo,Hamis Mwinjuma, mkuu wa mkoa wa Morogoro,Adam Kighoma Malima,mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Musa Kilakala,Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro,Paschal Kihanga

No comments:

Post a Comment