Breaking News

Sep 24, 2024

WAZEE KINGOLWIRA WAOMBA HUDUMA YA MATIBABU VITUO VYA AFYA UBORESHWE

 

WAZEE KINGOLWIRA WAOMBA HUDUMA YA MATIBABU VITUO VYA AFYA UBORESHWE

  • Viongozi wa CCM tawi la Legezamwendo Waunga Mkono Mchakato wa Bima ya Afya kwa Wazee

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

WAZEE wa Kata ya Kingolwira,Manispaa ya Morogoro wameiomba serikali kuwepo kwa Mkakati wa kutatua changamoto zinawasibu wazee ikiwemo urasimu wa upatikanaji wa huduma ya matibabu katika zahanati na vituo vya afya kwa kuwa hawana bima ya afya.

Katika Risala yao iliyosomwa na Katibu wa Baraza la Wazee Kata ya Kingolwira,Manispaa ya Morogoro,Scolastika Mluge mjini hapa,wazee wameonesha imani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha dhamira ya kutatua changamoto zinazowakabili wazee.

Mwenyekiti wa Baraza la wazee,Kata ya Kingolwira,Mapatano Mlay(Mwenye vazi la Pinki),kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Bomba la zambia,kata ya Kingolwira,Kabonga Adolf ambaye akimwakilisha Diwani wa Kata ya Kingolwira.

Mbali na changamoto hiyo,Wazee hao wamesema wanakabiliwa pia na huduma nyingine za kibinadamu chakula na mavazi,hivyo wameiomba watu wenye mapenzi mema kujitokeza kuwasaidia kwa kuwasiliana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kingolwira ambaye ndio mlezi wao.

Viongozi wa Baraza la Wazee wakishiriki kukata keki na Mtendaji wa Kata ya Kingolwira,Esther Shayo,katika hafla ya siku ya wazee duniani iliyofanyika katika eneo la Kata ya Kingolwira,Manispaa ya Morogoro

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kingolwira, Esther Shayo amewaasa wamewahakikishia wazee hao kuwa serikali inatambua mchango waliutoa katika kulijenga taifa,hivyo changamoto walizozianisha zitafanyiwa kazi kwa kufikisha katika ngazi za juu za kimamlaka.

Shayo amesema kuwa wakati taifa inaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unatarajia kufanyika Novemba 27,mwaka huu,amewahimiza wazee kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi huo muda utakapofika kwa kuwa serikali imeaandaa utaratibu maalum kwa wazee na makundi maalum kupiga kura.

Mtendaji wa kata ya Kingolwira,Esther Shayo kulia,kushoto kwake ni Scolastica Mluge,Katibu wa Baraza la Wazee Kata ya Kingolwira wakati wa Maazimisho ya siku ya wazee Duniani

Mzee Kabonga Adolf ambaye ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa ya   Bomba la Zambia, alimwakilisha Diwani wa Kata ya Kingolwira, Madaraka Bidyanguze alisema kuwa changamoto zinazowakabili wazee wa eneo hilo zitafanyiwa kazi hususan urasimu wanaoupata wakati wa kwenda katika vituo vya kutolea huduma ya afya

Baadhi ya wazee wa kata ya Kingolwira walioshiriki katika hafla ya siku ya wazee duniani

Kata ya Kingolwira  ina jumla ya 8 ambayo ni Mtaa wa Zahanati,seminari,Mahakamani,,tambuka Reli,Tangi la Maji,Shule,bomba la Zambia na Mwembemsafa ambapo wananchi wa maeneo hayo wameaswa kuzingatia maelekezo ya serikali ili kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa katika maeneo hayo yanakuwa amani na utulivu.

Katika maadhimisho hayo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na viongozi wa siasa,mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na viongozi wa serikali na baraza la wazee kutoka maeneo ya jirani.

Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Tawi la CCM,Tawi la Legezamwendo,Mohamed Matata,ambapo aliongozana na katibu wake wa tawi,Yusufu Mkuki ambao walionesha ushirikiano kwa wazee hao kwa kuchangia mchakato wa bima ya afya kwa kuwalisha keki wazee 20 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mchakato huo.

Mwenyekiti wa CCM tawi la legazamwendo,Mohamed Matata,kushoto akiwa na katibu wake,Yusufu Mkuki wakiwa na nyuso zenye kutafakarisha namna ya kuwaunga mkono wazee wa Kingolwira ambao inakadiriwa kuwa 250 waliopo katika kata hiyo.

No comments:

Post a Comment