Breaking News

Sep 24, 2024

BENKI YA NMB YAKABIDHI SHIMIWI VIFAA VYA MICHEZO VYA MIL.24.5

 

BENKI YA NMB YAKABIDHI SHIMIWI VIFAA VYA MICHEZO  VYA MIL.24.5

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

KATIKA kuhakikisha michezo katika taasisi na idara za serikali zinaendelezwa kwa watumishi wa umma zaidi 2500 wamepatiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi mil.24.5 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.

Meneja Mwandamizi wa huduma za kibenki na mahusiano kwa upande wa serikali kuu,Amanda Feruzi aliyesimama akisisitiza jambo katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa uongozi wa shimiwi.

Meneja Mwandamizi wa huduma za kibenki na mahusiano kwa upande wa serikali kuu,Amanda Feruzi amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo benki ya NMB imekuwa ikishirikiana na shimiwi katika kuendeleza michezo kwa kwa kutoa vifaa vya michezo.

Feruzi amesema kuwa mahusiano yaliopo baina ya taasisi hiyo ya fedha na serikali hayaishi tu kwenye shughuli za kibiashara bali pia kwenye michezo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika mikakati yake ya kuendeleza michezo.

“ Kauli ya Rais wakati akiingia madarakani alikuwa akisisitiza michezo na suala la kujenga afya  kwa sababu michezo ni afya na sisi tunaunga mkono juhudi hizo kwa kushirikiana na shimiwi.”alisema

Awali akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na idara za Serikali,Michael Masubo amesema uzinduzi rasmi wa mashindano hayo ya SHIMIWI unafunguliwa Septemba 25, mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro na mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ni Naibu Waziri Mkuu,Dkt.Doto Buteko.

Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na idara za Serikali,Michael Masubo akitoa neno katika hafla ya makabidhiano

Masubo amesema michezo mbalimbali inayotarajiwa kufanyika katika mashindano hayo ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, mpira wa pete, netball, mashindano ya kukimbia  na michezo mingine ya Jadi.

Aidha,alishukuru taasisi hiyo ya fedha kwa mkakati wake wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuendeleza michezo katika wizara na idara za serikali ili kuleta chachu na ari ya kupenda kufanya mazoezi kwa kuwa michezo ina faida kubwa kiafya.

Meneja Mwandamizi wa huduma za kibenki na mahusiano kwa upande wa serikali kuu,Amanda Feruzi(kushoto) akimkabidhi Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na idara za Serikali,Michael Masubo vifaa vya michezo kwa ajili ya watumishi wa Wizara na idara za serikali

“Michezo hii itafanyika kwa siku 14 hadi 16 katika uwanja wa Jamhuri kuanzia tarehe 25 septemba hadi oktoba 5 mwaka huu”alisema Masubo

No comments:

Post a Comment