MADIWANI MOROGORO WAMPITISHA KWA KISHINDO SEIF CHOMOKA NAIBU MEYA
Na Thadei Hafigwa
BARAZA la
Madiwani,Manispaa ya Morogoro lenye wajumbe 42 kwa kauli moja wamemthibitisha Diwani
wa kata ya Mkundi,Seif Chomoka kuwa naibu Meya wa Halmashauri hiyo atakayeongozwa
kuwa kipindi cha mwaka moja kutokana na imani kubwa waliyonayo dhidi yake.
Katibu wa Baraza la
Madiwani ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro,
Emanuel Mkongo Kabla ya baraza hilo kumdhibitisha alisoma barua kutoka chama
cha mapinduzi Wilaya ya Morogoro mjini inayoelezea jina la Seif chomoka ambaye
alishinda uchaguzi wa naibu meya katika chama hicho.
Baada ya waraka huo wa CCM kusomwa,Meya ya
Manispaa ya Morogoro,Paschal Kihanga alitoa fursa kwa madiwani kumthibitisha
jina la Seif Chomoka kushika nafasi hiyo ambayo hapo awali ilishikiliwa na
Mohamed Lukwele ambaye katika uchaguzi ndani chama cha Mapinduzi alipata kura 15 huku Seif Chomoka aliinuka kwa kupata kura 23.
Mara baada ya
kuthibitishwa,Seif Chomoka katika hotuba yake ya shukrani aliahidi kufanyakazi
kwa uadilifu kwa kushirikiana na Meya na menejimenti ya halmashauri ya Manispaa
ya Morogoro ili kuhakikisha kasi ya maendeleo ya wananchi inaongeza na
kupunguza kero zinazowakabili wananchi wa manispaa hiyo.
Aidha,Chomoka
aliwashauri ofisi ya Mkurugenzi wa
Manispaa kutafuta uwezekano wa kuongeza samani za ofisi za kisasa ili madiwani
waweze kutimiza wajibu wao katika mazingira rafiki badala ya kutumia viti vya
plastiki kwenye vikao vyao.
Katika baraza hilo pia
walifanya uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbalimbali iliwemo kamati za kudumu
ya mbili za kudumu,kamati za mipango miji,ambaye mwenyekiti wake ni Amin
Tunda,Diwani wa Kata ya Kingo ambayo ndani ya kamati hiyo kuna kamati ndogo ya
mazingira ambaye mwenyekiti wake ni Rashid Matesa,Diwani wa kata ya Uwanja wa
Taifa.
Kamati nyingine ni kamati
ya huduma za jamii,elimu na afya ambaye mweyekiti wake ni Majuto Mbuguyu,Diwani
wa kata ya Uwanja wa Ndege katika kamati hiyo kuna kamati ndogo ya afya ambaye
mwenyekiti wake ni Samuel Msuya,Diwani wa Kata ya Mbuyuni ambaye alichaguliwa
bila ya upinzani.
No comments:
Post a Comment