RC Malima:Msimu ujao wa Sherehe ya Nanenane Kanda Mashariki Kuboreshwa
Na Thadei Hafigwa,Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro,Adam Kighoma Malima amesema ya Maonesho ya Wakulima,Wavuvi na
Wafugaji,Nanenane kanda ya mashariki yataboreshwa zaidi katika Msimu ujayo ili
kuleta tija kwa wananchi.
Malima amesema hayo wakati
wa kilele cha maonesho ya wakulima,wavuvi na wafugaji katika viwanja cha
Mwalimu Nyerere ikiwa ni sehemu ya tathmini ya awali ya maadhimisho ya msimu
kwa mwaka huu,2023.
Alisema kuwa zipo changamoto
zilizojitokeza katika maonesho ya mwaka 2023,kwamba mkakati uliopo ni kuanza
kufanya maandalizi mapema ifikapo mwezi januari ili maonesho hayo yawe endelevu
na tija kwa wananchi.
Katika Kilele cha Maonesho ya nanenane kanda ya mashariki mgeni rasmi
alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba amewataka wakulima kuwa na
uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo ili kukidhi
mahitaji ya nchi na kupanua na kukidhi soko la biashara za mazao yatokanayo na
mazao,mifugo na uvuvi.
Kindamba kabla ya kuhutubia wananchi aliweza kutembelea mabanda
mbalimbali ambapo alishuhudia kuwepo kwa teknolojia na zana za kilimo, ufugaji na
uvuvi ambapo aliwahimiza kuendelea kuongeza ubunifu kwa msilahi mapana na jamii
ya kitanzania mijini na vijijini.
Katika maadhimisho hayo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ilibuka
kidedea katika halmashauri zilizopo katika mkoa wa Morogoro na kufuatiwa na
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambayo ilipata ngao.
Aidha,Bodi ya Sukari
imekuwa ni mshindi wa jumla kwa kufanikiwa kufanya vizuri na kuwashinda
washiriki wengine ambao walihimizwa kuongeza bidii katika msimu mwingine ili
kuongeza ushindani wenye masilahi mapana kwa wananchi.
Kindamba ametaja changamoto kuu iliyojitokeza
katika msimu wa Nanenane 2023 ni upungufu wa maji,jambo ambalo limeathiri
vipando kumea vema,hivyo ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha miundombinu
ya maji yanaboreshwa katika kipindi kijacho.
Sherehe za nanenane kanda ya mashariki ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani.Kunenge,Mameya,madiwani,wakuu wa taasisi za umma pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali yaliopo kanda ya mashariki inayojumuisha mikoa ya Morogoro,Pwani,Dar es Salaam na Tanga.
No comments:
Post a Comment