Zaidi ya Sh.bil 1 ya mfuko wa sanaa yawanufaisha walengwa 45 nchini
MFUKO wa sanaa na utamaduni
toka ulipozinduliwa Desemba 23,2023 umeweza kutoa mikopo wenye thamani ya
shilingi bil.1.07 na kuweza kuwanufaisha wadau wa tasnia ya sanaa 45 wakiwemo
walemavu.
Mtendaji Mkuu wa mfuko wa
Sanaa na Utamaduni Tanzania,Nyakoho Mahemba amebainisha hayo mijini Morogoro
wakati wa warsha kwa wadau wa sanaa na utamaduni,aliongeza kuwa mbali ya kutoa lengo
la mfuko huo ni kutoa huduma za mikopo ya urejeshaji ili kuendeleza tasnia ya
sanaa hana nchini baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto ya mitaji kwa wasanii.
Mahemba amesema kwamba mfumo
huo pia unatoa mikopo wa vifaa na vitendea kazi kwenye tasnia hiyo,ambapo
miongoni mwa wanufaika ni kundi la walemavu walipatiwa mkopo wa shilingi mil.55
kwa ajili ya kuwaendeleza walemavu wenzao kwenye tasnia ya sanaa hususan
tamthiliya,kuibua vipaji na kuwawezesha watoto wanaoishi kwenye mazingira
magumu.
Amesema kuwa,Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye watu wenye vipaji vya sanaa jambo ambalo limewasukuma kuwapa mafunzo wasanii waliopo katika mkoa huo ili kuhakikisha wapata uwelewa wa kuandika miradi na mchanganuo utakaowaweka kwenye mazingira rafiki ya kukopesheka na taasisi za fedha.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na sanaa,Bi.Nyakoho Mahembe(Katikati) akifwa na Afisa Elimu Taaluma,Mkoa wa Morogoro,Bw.Tullo Fundi (Kulia)wakati warsha ya siku moja kwa wasanii wa Morogoro juu ya fursa ya mkopo unaotolewa na mfuko wa Utamaduni na Sanaa hapa nchini.“Mfuko unatoa mkopo wa
kujikimu au dharura ambayo ni ya muda mrefu kwa lengo la kujikimu wakati wa
safari za kuandaa au kufanikisha mambo ya sanaa aidha ndani au nje ya
nchi”amesema.
Ametaja miongoni mwa
manufaa yaliyopatikana na uwepo kwa mfuko huo ni kufanikisha kuwa na Studio 21 zenye vifaa vya kisasa za kurekodi kazi za
sanaa na hivyo kuwarahisishia wasanii hapa nchini badala ya kwenda nje ya nchi
huduma hiyo wanaipata nchini na kukuwapunguzia gharama za kusafiri ughaibuni.
“mfuko huu sasa ni kichocheo
cha uchumi katika sekta ya utamaduni na sanaa kwa kuigeuza sekta hii biashara
na kuleta tija kwa wananchi wakiwemo wakazi wa Morogoro” alisema
Aidha,alitaja changamoto
zinazowakabili wasanii na wadau wa utamaduni ni kutokuwa na elimu ya fedha na usimamizi wa
miradi hivyo ili kukabiliana na hali hiyo wameona kuna haja ya kutoa mafunzo
ili wadau watakaopata mikopo waweze kurejesha na mfuko kuwa endelevu.
Kwa upande wake,Afisa
Utamaduni Manispaa ya Morogoro,Safia Kigwahi amesema ofisi yake itahakikisha ya
kuwa wasanii na wadau wa utamaduni wanakuwa na uwelewa wa kutosha.
Warsha hiyo ilifunguliwa na
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt.Mussa Ali Mussa alipongeza sekta binafsi
kushirikiana na serikali katika kuchangia pato la taifa ili hali inayochangia
kusukuma maendeleo ya nchi.
Akisoma hotuba kwa niaba ya
Katibu Tawala,Tullo Fundi,Afisa Elimu na Taaluma mkoa wa Morogoro alitoa wito
kwa wasanii waliopo mkoa wa Morogoro kuchangamkia fursa ya mikopo na kurejesha
kwa wakati ili adhima ya serikali ya kuwafikia walengwa inatimia.
Dkt.Mussa pamoja na mambo
mengine amesema kwamba,ni jukumu la kutumia fursa hiyo ili kuondokana na kwamba
sanaa badala ya kustarehesha na kuwa na kuwa fursa ya kiuchumi na kibiashara.
Mafunzo hayo yalishirikisha viongozi mbalimbali katika ngazi ya kitaifa akiwemo raisi wa shirikisho la sanaa za fundi stadi Tanzania,Adrian Nyangamalle na Dkt.Cynthia Henjewele,raisi wa Shirikisho la Maonyesho Tanzania(SHISAMA)
No comments:
Post a Comment