Breaking News

May 25, 2021

WAVUVI WADOGO WATOA ‘NYONGO’ WACHOCHWA UBABE WA MAAFISA UVUVI

 WAVUVI WADOGO WATOA ‘NYONGO’ WACHOCHWA UBABE WA MAAFISA UVUVI

Na Lilian Lucas,Morogoro.        

WAVUVI wadogo nchini wamedai wamekuwa wakishindwa kuweka wazi takwimu za mavuno yatokanayo na uvuvi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubabe wanaofanyiwa na baadhi ya Maafisa Uvuvi, hofu ya kuadhibiwa au kutozwa faini zinazosababisha kupoteza mapato sambamba na uchache wa maafisa uvuvi na wakusanya takwimu katika maeneo yao.

Walieleza hayo wakati wa mkutano wa wadau wenye lengo la kupitia matokeo ya utafiti wa mchanganuo wa wavuvi wadogo nchini uliofanyika mjini Morogoro.

Mvuvi kutoka Nyasa Mkoani Ruvuma Peter Sumuni alisema kuwa wavuvi na maafisa uvuvi kwa ujumla wamekuwa maadui badala ya kuwa marafiki , mara zote wavuvi wanapofuatwa na maafisa hao wanachofikiria ni kupigwa faini na adhabu mbalimbali.

“Hii imekuwa kama wanyamapori wanapomuona muindaji muda wote wanafikiria na kuwaza kukimbia kwa kuhofia kuuwawa, kwa hiyo mvuvi muda wote anajihisi yeye ni wa kukosea tu hilo ndilo linapelekea mvuvi kutoa data zisizo sahihi,”alisema.

Aidha Sumuni alisema hata kama mvuvi atapata mafanikio mkubwa lazime apuuze, na kwamba maafisa uvuvi wamekuwa hawafiki maeneo husika ya wavuvi kutokana na kuwa wachache jambo linalowafanya kutopata takwimu sahihi.

Alitolea mfano kwa eneo la wilaya ya Nyasa maafisa hao wapo wawili na kuwamekuwa ni moja na ndilo wanapofika na kupata takwimu na kuziwasilisha na kuchukulia wastani na maeneo mengine hayafikiki namna ya kuzipata inakuwa tatizo.

“Makadirio lazima yawe ya chini ukilinganisha na wingi wa watu na wingi wa wavuvi, mfano mwaka 2018 tumepata taarifa kwamba Ziwa Nyasa mazao ya uvuvi wa dagaa yamepatikana kilo tisa yaliyoenda nje ya nchi kitu ambacho ni kituko lakini tunaamini hilo linawezekana au pengine haliwezekani,”alisema.

Alisema kutokana na kutokuwepo kwa ushirikiano kumekuwa kukichangia wavuvi kupitisha mazao hayo ya uvuvi wamekuwa wakipiitisha kwa njia ya panya, adhabu na faini zimekuwa nyingi ni kutokana na maafisa kutotoa maelekezo kwa karibu kwa wavuvi na kuwafanya kuishi kwa mashaka.

Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Akwa ya Teknolojia ya Uvuvi Dk Paul Onyango alisema kutokana na matokeo ya Utafiti yaliyofanyika tangu 2018 hadi 2020 yaliyolenga kutathimini uvuvi mdogo Tanzania na kwamba nchi karibu 40 zimefanyiwa utafiti kama huo kwa ufadhili wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa(FAO) hasa kwa upande wa samaki.

Dk Onyango alisema kuwa matokeo hasa yaliyoonekana katika utafiti ni kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa data na hiyo ni kutoelewa umuhimu wa uvuvi mdogo katika nchi.

Alisema asilimia 99 ya uvuvi kulingana na takwimu za wizara na zile ya zingine ukiangalia kulingana na utafiti inatoa taswira kuwa mengi hayajafahamika na hayapatikani vyema kutokana na kutokuwepo kwa ukusanyaji sahihi wa takwimu hiyo.

Aidha alisema katika nchi nyingi za Afrika bado hakijafikia kiwango ambacho takwimu zinapatikana kwa usahihi na kwamba samaki imekuwa ikichangia kwa kiwango kikubwa kwenye chakula bora na kwamba ulaji wa dagaa ni mboga ambayo ni nzuri ukilinganisha na mboga nyingine.

“Katika takwimu zetu tumengalia samaki wanaopatikana maeneo ya uvuvi, lakini hatuoni takwimu ambazo zinaonyesha value ya samaki baada ya kutoka sehemu ambazo uvuvi unafanyika,”alisema.

Pia alisema kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha serikali inafanya uwezeshaji wa upatikanaji wa takwimu kutoka kwa wakusanyaji takwimu, ambapo alipendekeza Wizara ya Mifugo kwa makusudi iweze kutenga bajeti maalumu kwa ajili ya ukusanyaji takwimu kuanzia kwenye halmashauri, kuwepo kwa watu maalumu wa kukusanya, wavuvi waombwe kujitolea kutoa takwimu zao sahihi kwa hiari ili kusaidia Serikali kuweka mkakati wa maendeleo katika sekta ya uvuvi

Mwakilishi wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) idara ta uratibu na sera,Yusuph Semguruka alieleza kuwa mikakati ya serikali kuongeza ajira kwenye sekra ya uvuvi ambapo alisema kama itatekelezeka ipasavyo suala la ukusanyaji takwimu utaweza kupata ufumbuzi.

Aidha alisema ni vyema ili kuweza kupatikana na takwimu maafisa uvuvi waangaliwe kwa jicho la kipekee na kuwezeshwa kufika kwenye maeneo yasiyofikika ili awaweze kufanyakazi kwa uafanishi na kuepuka changamoto zilizopo kwenye sekata ya uvuvi.

Upande Sekta ya Uvuvi imekuwa ikichangia pato la taifa kwa asilimia 1.7 hivyo kama takwimu sahihi itapatikana itasaidia kuongeza pato hilo kwa kasi kubwa.

No comments:

Post a Comment