Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo
CHONGOLO AWAASA VIONGOZI PWANI KUACHA
VIKAO VISIVYO NA TIJA
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Choholo alitoa rai hiyo wakati alipofanya
ziara ya kujitambulisha toka alipoteuliwa kuwa katibu mkuu wa chama cha
mapinduzi taifa ikiwa ni hatua ya kuendeleza utekelezaji wa ilani ya chama
hicho ya 2020-2025.
Alisema kuwa angependa kuona viongozi
katika ngazi mbalimbali wanafanyakazi kwa bidii na kuacha tabia ya kuseng’enyana
ikiwa ni hatua ya kusukuma maendeleo ya
wananchi ambao wanaimani kubwa na chama cha mapinduzi
Aidha,ziara ya katibu Mkuu aliambatana na
Sekretarieti ya Chama hicho kwa ajili ya kuweza kujitambulisha kwa
wanachama na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti
wa halmashauri pamoja na viongozi wa ngazi ya Mkoa wa Pwani,ambapo Naibu Katibu
Mkuu Bara Christina Mdeme, amezitaka Jumuiya za chama hicho kufanyia kazi
maadili ya Vijana.
Alisema Jumuiya ya Wazazi, Wanawake na Vijana zinatakiwa kufanya
kazi kwa kuzingatia maadili ya Vijana kwa kuwaenzi wazee.
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema viongozi wa chama hicho
wanatakiwa kufanya kazi kwa vitendo na si kwenye televisheni na mitandao ya
kijamii.
"Kamati za siasa zitenge muda wa kukagua miradi na
kutoa ushauri, lakini pia iwepo siku moja ya kusikiliza kero za Wananchi"
alisema Mndeme.
Kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka
ameahidi kuyatekeleza maagizo yote ambayo yametolewa na Katibu mkuu wa Chama
cha mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ikiwemo kusimamia suala zima na
utekelezaji wa ilani ya chama kwa kuhakikisha anasikiliza kero mbali
mbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ikiwemo kulivalia njuga suala
la kukithiri kwa mashamba pori lengo ikiwa ni kuleta chachu ya maendeleo kwa
wananchi.
Koka alisema kwamba ujio wa Katibu huyo katika Mkoa wa Pwani
umeweza kuleta neema zaidi kutokana na maelekezo ambayo yametolewa ya
kuwakumbusha viongozi mbalimbali wa chama kuweza kutekeleza majukumu yao
ipasavyo na kuchapa kazi kwa bidii ikiwa ni kutekeleza miradi ya
maendeleo ambayo ipo katika ilani ya chama cha mapinduzi.
No comments:
Post a Comment