NA
VICTOR MASANGU, RUFIJI
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhe.
Aboubakar Kunenge amekerwa na madhaifu kwa baadhi ya watendaji kutokuwa na
tabia ya ucheleweshwaji wa Pembejeo za kilimo hali ambayo inawakwamisha
wakulima kutoweza kufanya shughuli zao za kilimo kwa ufanisi ambao unatakiwa.
Kunenge
ametoa kauli hiyo wakati akiendesha kikao cha wadau wa zao la Ufuta
kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha ufundi stadi (FDC) Wilayani Rufiji ambapo
kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na viongozi wengine
wa serikali wa ngazi za Wilaya na Mkoa.
Pia, Mkuu aliongeza kuwa anasikitishwa sana na kuona
baadhi ya watendaji na viongozi wengine kuwa na urasimu na kuwataka wabadilike
na kuhakikisha kwamba wanaweka mikakati madhubuti ambayo itawasaidia wakulima
hao waweze kulima kilimo chao amabcho kina tija katika Mkoa wa Pwani.
“Kwa
kweli kwa upande wangu nina kerwa sana na madhaifu ambayo yanafanywa na
baadhi ya watendaji wetu, jambo hilo sio sawa kabisa hata kidogo na wengine
bado wana tabia ya kufanya urasarimu lakini lengo letu sisi ni kuona wakulima
wa zao la ufuta kwa kushirikiana na serikali wanalima kilimo chenye
tija.”alisema Kunenge.
Kadhalika aliwataka viongozi kuweka mpango kabambe ambao utaweza
kuondokana na changamoto ya uhaba wa vifungashio vya ufuta na kwamba ataendelea
kuwapa ushirikiano wa kutosha ili waweze kutimiza malengo yao waliyojiwekea.
Pia
Kunenge aliongeza kuwa katika kuwasaidia wakulima wa zao la ufuta kunahitajika
ushirikiano madhubuti kutoka kwa wadau mbalimbali wa zao hilo ili kuweza
kusimamia zoezi zima la uendeshaji wa mnada wa kwanza bila ya kuwa
na ucheleweshwaji wowote.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa aliwataaka wakulima wote
kulima kilimo chenye Tija, na kuahidi kuwa serikali ya awamu ya sita ipo
tayari kuwasaidia ili waweze kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa na
chenye kuleta mafanikio kwa Mkoa.
Kungene katika kikao hicho aliwaagiza Wataalamu mbalimbali wa
kilimo pamoja na Ofisi yake kufanya Tathmini ya zao hilo na kuja na
Mkakati endelevu ambao utaleta matokeo chanya katika suala zima la kukuza
kilimo cha zao la ufuta katika Mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment