MKUU WA MKOA WA PWANI,ABOUBAKAR KUNENGE AKIVISHWA SKAFU NA KIJANA WA SKAUTI MARA BAADA YA KUWASILI WILAYA NA BAGAMOYO KWA ZIARA YA KUJITAMBULISHA
KUNENGE ACHANJA MBUGA, AWASILI
BAGAMOYO AWAASA WATUMISHI
NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
MKUU wa Mkoa wa Pwani Mh. Aboubakar Kunenge
amewataka wataalamu na watumishi wa halmashauri ya Bagamoyo kuhakikisha
wanafanya kazi kwa weledi na kutumia ujuzi walionao katika kukabiliana na
changamoto zinazowakabili katika maeno yao ya kazi na kutumia fursa zilizopo
katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kunenge ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika halmashauri
ya Bagamoyo kwa lengo la kuweza kujitambulisha pamoja na kuzungumza na baadhi
ya watumishi wakuu wa idara pamoja na wataalamu kwa lengo la kuweza kupeana
maelekezo katika suala zima zima uwajibikaji.
Aidha kunenge katika kikao hicho amewakumbusha wataalamu
kuhakikisha kwamba wanaweka mikakati madhubuti katika suala zima la ukusanyaji
wa mapato kwa lengo la kuwez kuwaletea wananchi maendeleo.
“Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Rais wa awamu ya
sita Mama Samia Suluhu kwa kuweza kuniamini tena naa kunipanafasi ya kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Pwani lakini lengo langu kubwa nimekuja kuwasalimia ili tuweze
kuweka miapango madhubuti ambayo itasaidia katika kuleta chachu ya maendeleo
katika maeneo yetu.”alisema Kunenge.
Aidha Kunenga aliwataka wataalamu mbalimbali kujenga tabia ya
kufanya utafiti ambao utawasaidia katika kubaini fursa mbali mbali zilizopo
katika maeneo yao kwa lengo la kuweza kuzitumia kikamilifu ili ziweze kuleta
matokeo chanya na mafanikio katika maeneo ambayo wanayafanyia kazi.
Pia alibainisha kwmaba watumishi na waattalamu wanatakiwa
kushirikiana bega kwa bega katika Nyanja mbali mbali na kuzitafutia ufumbuzi
changamoto zilizopo ilengo ikiwa ni kuweka mipango madhubuti ambyo itaweza
kuzaa matunda katika siku za usoni na kwamba lengo la serikali ni kuwaletea
wananchi maendeleo.
Kadhalika Kunenge alisema kwamba lengo la serikali iliyopo
madarakani ni serikali ya Chama cha mapinduzi (CCM) hivyo ni lazima itatekeleza
Ilani ya Chama katika ni kuhakikisha inatumikia wananchi wananchi na
kuzisikiliza kero na changamoto zao mbali mbali zinazowakabili.
“Kitu kikubwa ambacho nina kiomba kwa watumishi wote wa umma ni
lazima kuweka mikakati ya kutekeleza ilani ya cahama cha mapinduzi kwa vitendo
kwa serikali hii ndio inasimamiwa na CCM na kwamba ni lazima watumishi wote kw
akipindi hiki inapaswa kchapa kazi kweli kweli kwa bidii ili tuweze
kutumiza yale yote amabyo yameelekezwa katika Ilani ya Chama.
Katika hatua nyingine Kunenge aliongeza kwamba atahakikisha
kwamba anashirikiana na viongozi mbali mbali wakiwemo wakuuu wa wilaya
wakurugenzi ili kuweza kufikia lengo ambalo limekusudiwa na serikali katika
kuwatumikia wananchi pamoja na kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Awali kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa
akisoma taarifa ya Wilaya hiyo, alisema kwa sasa bado kuna changamoto mbali
mbali ambazo zinatakiwa zifanyiwe kazi ikiwemo kukithiri kwa uwepo wa
bandari bubu 19 ambazo zimekuwa zikitumika katika kufanyia biashara za magendo.
Aidha, Kawawa aliongeza kwa sasa katika kukabiliana na
changamoto hiyo wameshaanza kufanya doria katika bahari ya hindi kwa lengo la
kuwabaini wale wote ambao wanahusika na matukio
ya kiuharifu kupitia bandari hizo bubu.
No comments:
Post a Comment