Breaking News

May 25, 2021

CAMFED TANZANIA YATAJA ATHARI ZA KIELIMU WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU

CAMFED TZ YATAJA ATHARI ZA KIELIMU WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU

Lilian Lucas,Morogoro.

Imeelezwa sababu moja wapo ya kuwafanya watoto wanaishi kwenye mazingira magumu kukosa Elimu bora na kutokana na kusoma kwa kuregarega, utoro, umaskini na kuacha shule.

Mkurugenzi wa Shirika la Camfed Tanzania Lydia Wilbard alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara ya kukutana na wadau wa Elimu kwenye kikao kazi cha kujadili watoto wanaishi kwenye mazingira magumu na sababu za kuwafanya kukosa Elimu Bora.

Alisema katika kuhakikisha mtoto analindwa na kuheshimiwa katika jamii shirika limeona ni vyema likawaandaa watoto hasa walioko mashuleni kwa kuwapatia ujuzi wa ziada tangu wakiwa wadogo ili waweze kuweka malengo yao kwa kuishirikisha jamii na walimu pale wanaposoma.

Wilbard alisema progaramu ya Campaign For Female Education, imekuwa na msaada mkubwa kwa wanafunzi hasa wa kike ambao wamekuwa wakipata matatizo katika jamii inayowazunguka kwa kupata mimba na kuwafanya kuacha shule kutokana na mazingira magumu aliyopo(maisha anayoyaishi).

“Hii progaramu imeonyesha kwamba hawa watoto wa kike na kiume hasa wanaotoka kwenye mazingira magumu wakipata stadi za maisha ambazo zinaonyesha ili uwe bora katika dunia lazima uwe na uwajibikaji wa pamoja kwenye jamii imesaidia kuwajengea uwezo wa kujiamini, namna na kuongoza na kuondokana na umaskini, tumekuwa tukiwawezesha katika nyanja mbalimbali kama mafunzo ya biashara, ujasiliamami na kuwaunganisha na mifuko ya fedha ya uwezeshaji wa vijana inayotoka ofisi ya waziri mkuu na kuwawezesha kutengeneza ajita kwa wenzao,”alisema.

Alisema sababu kubwa ya watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu kwa utafiti wa shirkka hilo kuacha shule ni Umaskini na watoto wenyewe walieleza, kutojiamini kwamba anaweza kumaliza shule kama kutembea umbali mrefu hivyo shirika inachokifanya ni kuondoa kutojiamini ili aweze kumpa msukumo wa matamanio ya kujitambua na kujiwekea malengo.

Aidha alisema Shirika la Camfed mwaka 2016 ilipata nafasi ya kuungana na mchakato wa dunia ambao unaendeshwa na shirika la kimarekani likiwa na lengo la kuwaleta wadau hasa wa serikali ili kutathimini majibu ya changamoto zilizopo katika mfumo wa elimu na katika mfumo wa kuwaendeleza vijana kwenye mambo mbalimbali.

Mkurugenzi huyo alisema kikao hicho ni cha sita ambapo wamekuwa wakiunganisha wataalamu na wadau wa elimu kutoka kwenye wizara za Elimu, Tamisemi, Muunganiko wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanyakazi kwenye sekta ya elimu, maafisa elimu Halmashauri na lengo ni kuhakikisha mchakato wa kutengeneza program ya kifedha ambayo inaweza kufiki watoto wengi zaidi.

Alisema Shirika hilo linafanyakazi kwenye shule za Sekondari 455 mpaka sasa lakini program hiyo iko kwenye shule 407 ndani ya halmshauri 27, na kwamba lengo lao ni kufika kwenye shule zote Tanzania.

Alisema tangu kuanza kwa shirika hilo mwaka 2006 limeweza kusaidia watoto 48,205 moja kwa moja wa shule za Sekondari na walianza na watoto 28 kwa mkoa wa Iringa.

Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Morogoro Hatujuani Lukari alisema kuwepo kwa progaramu imesaidia watoto wa kike kujitambua na kutopata mimba akiwa shuleni na hiyo ni kuwawezesha na kuwaweka wazi.

“Elimu ya Dunia yangu bora imekuwa ikitolewa kwenye shule zote na wanafunzi wote wa kike na kiume na katika halmashauri yangu imesaidia na kuna kipindi kimoja kwa wiki wanapatiwa elimu ya utambuzi,”alisema.

“Mfano kwenye shule ya sekondari Mikese kila mwaka kulikuwa na watoto wa kike wawili wanapata mimba lakini baada ya kuwepo kwa progaramu hii kwa miaka miwili mfululizo hakuna mtoto aliyepata mimba,”alisema asifa elimu huyo.

 

 

No comments:

Post a Comment