JUKWAA LA WAHARIRI LAPATA VIONGOZI WAPYA
Na
Ashton Balaigwa,MOROGORO
JUKWAA la Waharri Tanzania (TEF) limemchagua Deodatus Balile,
kuwa Mwenyekiti mpya wa Jukwaa hilo ataongoza kwa kipindi cha miaka minne
ijayo baada kupata kura 57 dhidi ya mpinzani wake Neville Meena aliyepata
kura 22 katika uchaguzi uliofanyika mkoani Morogoro.
Balile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri,kabla
ya kushinda nafasi hiyo ya Uwenyekiti alikuwa Makamu mwenyekiti katika uongozi
uliomaliza muda wake.
Akitangaza matokeo hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Frank
Sanga, Wajumbe wa uchaguzi huo walikuwa 79 na hakuna kura iliyoharibika katika
nafasi ya mwenyekiti huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na
Bakari Machumu ambaye ni Mkurugenzi Mteandaji wa Kampuni ya Mwananchi kwa
kupata kura 53 na kumshinda Mpinzani wake Joyce Shebe kutoka Clauds Media
aliyepata kura 26.
Akizungumza baada ya kushinda nafasi hiyo,Balile alisema kwa
kushirikiana na viongozi wenzake anakusudia kufanya maboresho na kuongeza weledi
kwa waandishi habari ili kufanya uandishi usio wa harakati bali ulenge kusaidia
jamii kuleta maendeleo.
“ Uandishi wa habari sio uhanalakati bali ni kutumia wanyonge
katika kuibua matatizo yao yanayowakabili katika jamii yaweze kupata ufumbuzi “
alisema Balile.
Mikakati mingine ni pamoja na kuanzisha mafunzo kwa waandishi wa
habari ambao wanauzoefu wa muda mrefu lakini si wahariri ili kuwajengea uwezo
wa kufanya vizuri katika majukumu yao ya kila siku.
Naye Makamu Mwenyekiti ,Machumu,alisema uongozi ulioingia
madarakani utajieleza katika kuchochea maendeleo na kuwalea waandishi wa habari
na kuruhusu kupanua wigo kuwa na wanachama wengi kutoka katika Taasisi tofauti
tofauti ili kuleta maendeleo ya tasnia ya habari.
Katika nafasi ya wajumbe wa kamati tendaji waliochaguliwa ni
Salim Said Salim akitokea Zanzibar kura (75) Yassin Sadic
(69)Saimon Mkina(69)Jane Mihanji(63)Nevile Meena(62) Lilian Timbuka (55)
Angela Akilimali(48).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkutano huo Theophil
Makunga , aliwataka viongozi hao kutimiza ahadi zao walizotoa wakati wa
kampeni na kwenda kuimarisha TEF kwa maendeleo ya waandishi wa habari na tasnia
nzima ya habari hapa nchini.
Nae Msimamizi wa uchaguzi Mkuu wa TEF,ambaye ni Mkuu wa
Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Prudence Constantine,alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki hakuna
malalamiko.
No comments:
Post a Comment