Breaking News

Feb 2, 2021

TUJIKUMBUSHE MAELEKEZO YA SERIKALI KIPINDI CHA COVID 19

 

WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA,JINSIA,WAZEE NA WATOTO,DKT.DOROTHY GWAJIMA

TUJIKUMBUSHE MAELEKEZO YA SERIKALI KIPINDI CHA COVID 19

Na repota wetu,MOROPC BLOG

SERIKALI ya Awamu ya Tano,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Dkt.John Pombe Magufuli Rais wa wanyonge,haikukaa kimya mara baada ya kubainika ya kuwa baadhi ya watanzania kuwapata maambukizi ya covid 19 mapema mwaka 2020.

Hatua iliyoichukua Tanzania ni pamoja na kufunga shule na taasisi za elimu ya juu kwa kipindi cha miezi mitatu,toka mwezi machi hadi juni 2020.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,kupitia Waziri wa Wizara hiyo,Mhe.Ummy Mwalimu ilifanya jitihada kubwa katika utoaji wa elimu kwa wananchi namna ya kukabiliana na corona.

Aidha,kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Magufuli aliwahimiza watanzania kushikamana na kuendelea kumuomba Mungu ili taifa lipaki moja na wananchi wawe salama,ambapo kila mtanzania mwa imani yake waliweza kufunga kwa siku tatu,Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.

Kutokana na Hamasa hiyo,watanzania waliingia kwenye sala na dua,misikitini na makanisani,pia watanzania waliendelea kuchukua tahadhali dhidi ya corona.

Kwa Mwaka jana 2020,Taifa la Tanzania liliendelea kupata neema na Baraka zake kutoka kwa Mungu ambapo watanzania waliendelea kuchapa kazi licha ya kuwa mataifa makubwa duniani yakiendelea kupambana na  covid 19.

Kwa mwaka 2021,corona duniani imekuibuka katika kura nyingine ambapo viongozi wa serikali akiwemo Rais Magufuli aliwakumbusha watanzania kuendelea kuchukua tahadhali,na kuendelea kutumia silaha iliyotumika kwaka jana ya kupambana na covid 19,sala na dua

Pia,Waziri wa  Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto naye Dkt.Dorothy Gwajima,aliwakumbusha hivi karibuni waandishi wa habari na taasisi za dini na wadau wa maendeleo kuendelea kuwaelimisha wananchi kujihadhali na covid 19 bila ya kuwasababishia taharuki.

Msemaji wa Serikali,Dk.Hassan Abbas naye Kwa upande wake alisema serikali ilishatoa mwongozo wake katika kukabiliana na covid 19 na magonwa mengine ya mlipuko,hivyo watanzania wanapaswa kuendelea kufuata maelekezo ya serikali.

No comments:

Post a Comment