Breaking News

Mar 10, 2021

OCODE YAWAKUTANISHA WADAU WA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

 

AFISA MAENDELEO YA JAMII,MANISPAA YA UBUNGO, ROSE MPELETA AFAFANUA JAMBO


OCODE YAWAKUTANISHA WADAU WA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

VICTOR MASANGU

SHIRIKA  lisilokuwa la kiserikali la Organization Community Development (OCODE) limeamua kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo katika Manispaa ya Ubungo lengo ikiwa ni kuweza kujadilina namna ya kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo pamoja na kuweka mipango mikakati ambayo itaweza kusaidia kuboresha sekta ya elimu kwa  wanafunzi shule wa shule za  msingi.

Hayo yamebainisha na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo la Ocode, Joseph Jackson wakati wa kikao maalumu cha wadau wa maendeleo mbalimbali  wa manispaa ya Ubungo kwa ajili ya kujadili changamoto  mbalimbali, kupanga mikakati pamoja na kuelezea taarifa ya utekelezaji wa mambo ambayo yamefanywa na  shirika hilo kwa kipindi kilichopita.

“Sisi kama shirika la Ocode lengo letu ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya  tano katika kuboresha sekta ya elimu, na kwamba leo tumeamua kuwakutanisha wadu wetu mbalimbali wa maendeleo katika manispaa ya Ubungo ili tuweze kutoa taarifa ya utekelezaji wetu kwa zile kazi mbali mbali ambazo tumezifanya katika shyule nne za msingi pamoja na kujadili changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja.

Aidha, Mkurugenzi huyo, alibainisha kwamba mradu huo wa elimu kwa sasa umeweza kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kuzisaidia shule nne za msingi kutoka Manispaa ya Ubungo kwa kuwasapoti kujenga miundombinu ya madarasa, madawati, viti, pamoja na miundombinu rafiki ya ngazi kwa ajili ya kuwasiadia watoto wenye mahitaji maalumu waweze kupita kwa urahisi bila ya kupata usumbufu wowote.

 Afisa  Maendeleo ya  jamii, Rose Mpeleta  ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi wa manispaa hiyo amebainisha kuwa walianza kufanya rasmi na shirika la Ocode tangu mwaka 2019 kwa lengo la kuweza kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi mbali mbali wa shule nne za msingi kwa kuzisaidia ujenzi wa madarasa, madawati pamoja na vifaa mbali mbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu.

“Sisi Kama manispaa ya Ubungo kwa kweli tunalipongeza Shirika hili la Ocode kwa kuweza kuunga juhudi za serikali katika kuinua na kuboressha sekta ya elimu na leo tupo hapa katika kikao cha wadau mbali mbali wa elimu lengo ikiwa ni kubadilishana mawazo ambayo yataweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika sekta ya elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Goba wakiwa wamekaa kwenye moja kati ya madawati yaliyotolewa na shirika la OCODE

Pia, alifafanua kwamba kupita mradi wa Ocode umeweza kuleta matokeo chanya  zaidi kutokana na kupunguza baadhi ya changamoto mbali mbali ambazo zilikuwepo katika baaadhi ya shule za msingi na kwamba  kwa sasa baadhi ya shule tayari zimeshanufaika na mradi huo ikiwemo sambamba walimu kupatiwa semina zinazohusina na elimu.

Naye mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Goba Ambrosi Mwakimbala amesema kwamba Shirika la Ocode limeweza kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo katika mambo mbali mbali ikiwemo ujenzi wa madarasa kwa ajili ya masomo ya awali na kwamba kwa sasa yameweza kuwa ni mkombozi mkubwa kuondokana na kukaa kwa mlundikano.

“Kwa kweli shirika hili la Ocode limeweza kutusaidia kwa kiais kikubwa  katika shule yetu hii ya msingi ya Goba kwani imetujengea ujenzi wa darasa kwa ajili ya watoto wa awali pamoja na kuweza kutupatia zana mbali mbali kwa ajili ya kufindishia lengo ikiwa ni kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi wa shule yetu,”alisema Mwalimu huyo.

Pia aliongeza kuwa katika kuboresha sekya ya elimu Ocode waliweza kuonyesha jitihada zao za dhati katika kutoa msaada wa kutoa madawati yapatayo 31 ambayo yameweza kusaidia kwa kiai kikubwa kupunguza adha ya wanafunzi kuondokana na wanafunzi kukaa kwa mlundikano na kwamba wameweza kuto mafunzo mbali mbali kwa walimu kwa lengo la kuwajengea uwezo katika suala zima la kutoa elimu ambayo ni jumuishi.

Kadhalika mwalimu huyo pia mbali la kulipongeza Shirika la Ocode amewaomba wadau mbali mbali wa maendeleo hasa katika sekta ya elimu  hasa akatika vifaa mbali mbali kwa ajili ya kuweza  kufundishia pamoja na kuwajengea vyumba vingine vya madarasa  ambavyo vitaweza kuwasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki.

SHIRIKA  lisilokuwa la kiresikali la Organization for Commmunity Development (OCODE) ambalo  kwa sasa limekuwa linafanya shughuli zake mbali mbali za kukuza sekta ya elimu katika Manispaa ya Ubungo lengo ikiwa ni kusiadia katika mambo ya ujenzi wa madarasa, kutoa vifaa vya kufundishia, kusaidia wanafunzi wenye mahitaji maaalumu pamoja na kutoa  semina kwa walimu wa shule za msingi.

No comments:

Post a Comment