RC PWANI
AKEMEA 'WANAUME' WANAOKATISHA WANAFUNZI MASOMO
NA
VICTOR MASANGU, PWANI
MKUU wa
Mkoa wa Pwani amechukizwa na kuwaonya vikali baadhi ya wanaume wenye tabia ya
kuwakatisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari masomo yao kutokana
na kuwapatia mimba na kushindwa kuendelea na masomo yao hali ambayo
amesema haikubaliki hata kidogo na kamwe hawezi kulifumbia macho suala hilo.
Mhandisi Ndikilo, alitoa kauli hiyo wakati akizungumza
katika maadhimisho na kilele cha siku ya mwanamke duniani ambapo kimkoa
zilifanyika katika eneo cha kimanzishana Wilayani Mkuranga na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa serikali, wabunge, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi viongozi
wa vyama vya siasa pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Alisema kwamba, kumekuwepo na baadhi ya wanafunzi katika Mkoa wa
Pwani ambao wanashindwa kufikia malengo ambayo waliyojiwekea kutokana na kupata
mimba hivyo jamii inatakiwa kulivalia njuga sula hili na kuhakikisha wanapiga
vita kabisa vitendo hivyo ambavyo vinachangia kwa kiasi kikubwa kuwanyima haki
yao ya msingi ya upatikanaji wa elimu.
“Kwa kweli jambo hili sio la kuvumilia kabisa hata kidogo lazima
sasa jamii yote kuwa kushirikiana na wawazazi na walezi katika Mkoa wa Pwani,
kulipiga vita haswa na sio kuliacha tuu kwa watoto wetu hawa kupata ujazuzito
na kutoshindwa kuendelea na masomo kwa hivyo mimi nasema hili jmbo halikubaliki
kabisa hata kidogo na ni lazima sasa tubadilike na kulipiga vita,”Alisema
Ndikilo.
Kadhalika Ndikilo, amekemea vitendo vya ukatili unaofanywa kwa
wanawake na kuwataka wakinababa kuchana kabisa na kuwanyanyasa wake zao kwa
kuamua kuwabaka,kuwatelekeza pamoja na kuwapiga bila sababu na badala yake
wametakiwa kubadilika kwa kuwaheshimu na kuwapa fursa mbalimbali ili wazeze
kuleta chachu ya maendeleo.
Pia, aliwaomba viongozi wa halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani
kuweka mipango madhubuti amabyo itaweza kusaidia kupunguza wimbi la wanafunzi
hao kupata mimba ambapo pia Wilaya ya Kisarawe ndiyo inayoongoza kwa kuwa na
idadi kubwa la ongezeko la watoto wa shule kupata ujauzito hivyo wanatakiwa
kulifanyia kazi jambo hilo.
“Kwa kweli wazai na walezi inabidi mbadilike kabisa inatakiwa
watoto wa kike wapatiwe fursa mbali mbali kwa ajili ya kupata muda mwingi
katika kusoma lengo ikiwa ni kutimiza ndoto zao amabzo wamezipanga na sio
kuwanyanyasa bila ya sababu za msingi hii inabidi muiache mara moja kwani sio
sahihi kabisa.”alisema Ndikilo.
“Jamani ndugu zangu hakuna masomo magumu katika shule hivyo kitu
kikubwa cha msingi wanafunzi wote wa kike pamoja na wale wa kiume
wanatakiwa wapewe nafasi sawa kwa ajili ya kusoma masomo yote bila ya
kuwabagua kwani watoto wa kike wanaweza kufanya mambo makubwa na kushika
nafasi mbali mbali za uongozi hivyo wanastahili kuwezeshwa ili waweze kutimiza
ndoto zao,”alisema.
Kwa Upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Pwani Dk. Delphine Magere
alibainisha kwamba lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba
inaendelea na jitihada madhubuti kwa ajili ya kuviwezesha vikundi mbali mbali
vya wakinamama katika mikopo ambayo inatolewa na halmashauri ili waweze
kujikwamua kiuchumi na kuleta chachu ya maendeleo.
Naye, Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa CCM Mkoa wa Pwani
Farida Mgome amempongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk.
Delphine Magere kwa kuwez kuwaunganisha wanawawe mbali mbali wa Mkoa huo katika
kujikita zaidi katika shughuli mbali mbali za uongozi pamoja na umahii wake
katika katika usimamizi mzuri wa shughuli mbali mbali za kiserikali.
“Kwa kweli sisi kama wanawake wa Mkoa wa Pwani
tunampongeza kwa dhati kabisa Katibu Tawala wetu wa Mkoa wa Pwani, kwani kwani
tangu aletwe hapa ameweza kuwa ni kiunganishi kikubwa katika kuwaongoza wananawake
wenake katika shuguli mbalimbali za kimaendeleo pamoja na zile nyingine za
kiserikali kwa kweli sisi tunajivunia sana na tunamtakia kila la kheri katika
utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku,”alisema Mwenyekiti huyo.
Kadhalika Mgomi, alisema kwamba anafarijika sana kuona ilani ya
Chama cha mapinduzi (CCM) inatekelezeka kwa kiasi kikubwa katika suala zima la
kuwawezesha wanaweke mikopo mbali mbali ambayo inawasaidia katika kijikwamua kiuchumi
na kupambana na wimbi la umasikini na kwamba wanawake ndio nguzo na msingi
mkubwa wa kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment