UNESCO yatoa tathmini ya
COVID-19 Sekta ya Elimu duniani
Peter Mgumia
SHIRIKA la Umoja wa
Mataifa la elimu (UNESCO) limebainisha kuwa zaidi ya wanafunzi milioni 800
ambao ni nusu ya wanafunzi wote duniani bado wanakabiliwa na changamoto kubwa
ya kufurugwa kwa ratiba ya masomo yao tangu kuzuka kwa janga la covid 19.
Kwa mujibu wa ripoti ya Elimu kutoka
Shirika hilo ikiwa ni sehemu ya tathmini ya athari ya covid duniani imabainisha
ya kuwa wanafunzi kote duniani wamefurugwa kwa elimu yaoikiwa ni theluthi 2 ya
mwaka wa masomo imepotea sababu ya covid 19.
“Wanafunzi milioni 800 ambao ni
zaidi ya nusu ya wanafunzi wote duniani bado wanakabiliwa changamoto kubwa ya
kuvurugwa kwa elimu yao, kuanzia kufungwa kwa shule katika nchi 31 hadi
kupunguzwa au kusoma kwa muda mfupi katika nchi zingine 48.”ilieleza sehemu ya
taarifa hiyo mpya ya UNESCO iliyotolewa hivi karibuni.
Wakati hayo yakijiri duniani,hapa
nchini wananchi wametakiwa kuchukua tahadhali kwa kuzingatia miongozo kutoka
wizara ya afya na maelekezo mengine ya kiserikali hali ambao imepokelewa kwa
mwitikio mkubwa kwa wananchi walio wengi kuvaa barakoa zinazozalishwa na
wajasiriamali wadogowadogo hususan mafundi cherahani.
Aidha,Wananchi wa Manispaa ya
Morogoro wameitikia wito wa serikali kwa kujali afya zao kwa kuweka ndogo za
kutakasa mikono kwa maji tiririka ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na magonjwa
ya mlipuko
Adili Omar ni miongoni mwa wakazi wa
manispaa ya Morogoro ameishukuru serikali kuendelea kuwahamasisha wananchi
kutokuwa na hofu na badala yake kuzingatia kanuni za afya ili jamii iendelee ya
kitanzania iendelee kuwa salama na kuchapa kazi.
No comments:
Post a Comment