Mkuu wa Shule ya msingi Kibwegere, Charles Kulemo kushoto akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi wa Shirika la Ocode ambao walifika shuleni hapo kwa ajili ya kuweza kukabidhi miundonbinu ya ya ngazi ambazo waliamua kuzijengwa kwa wajili ya kuweza kuwasaidia wanafunzi ambao ni walemamvu wa viungo.
OCODE 'YAPIGA JEKI' MIUNDOMBINU KWA WALEMAVU KIBAMBA
NA VICTOR MASANGU, KIBAMBA
KATIKA kuunga
mkono juhudi za serikali ya wamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu na
kuwathamini wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususan walemavu, Shirika
lisilokuwa la kiserikali la (OCODE ) limekuja na mpango kabambe ambapo limeweza
kuwasaidia baaadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibwegere
iliyopo kata ya Kibamba, kwa kuwapatia vifaa mbalimbali pamoja na kuwajengea
miundombinu rafiki ya majengo ili kuwarahisishia katika kutembea.
Akizungumza katika hafla fupi,
iliyoandaliwa kwa ajili ya kuweza kukabidhi baadhi ya miundombinu ambayo
imejengwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalumu,
Meneja wa anayesimamia miradi ya elimu katika Manispaa ya ubungo,
kutoka shirika la Ocode, Digna Mushi amebainisha kwamba utekelezaji
wa mradi huo wa kutoa vifaa pamoja na kuwajengea ngazi utakuwa ni mkombozi kwa
wanafunzi hao.
“Sisi Kama Shirika la Ocode tumekuwa tukifanya kazi ya mambo ya
elimu katika manispaa hii ya Ubungo lengo letu kubwa ni kuhakikisha watoto wetu
wanaweza kusoma katika mazingira rafiki, na leo hi tupo katika shule hii ya
msingi Kibwegere tumekuja kwa ajili ya kukabidhi miundombinu ya ngazi ambazo
zitaweza kutumika kwa wanafunzi mbalimbali ambao ni walemavu wa viungo tofauti
kama vile vya mikono pamoja na miguu sambamba pia kuwapatia vifaa vitakavyoweza
kuwasaidia,”alisema Digna.
Meneja Misimamizi wa miradi ya elimu katika Manispaa ya Ubungo
kutoka shirika la Ocode, Digna Mushi wa kushoto akipeana mkono na
Mkuu wa shule ya msingi Kibwegere Charles Kulemo iliyopo kata ya Kibamba
ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa miundombinu ya ngazi maalumu (hazipo pichani )ambazo
zitatumika katika kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususan walemavu
wa viungo kuweza kupita kwa urahisi pindi wanapokwenda madarasani.
Naye, Mkuu wa shule ya msingi Kibwegere, Charles Kulemo
amesema kwamba wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo wapo 15 na
kwamba msaada huo wa walioupata kutoka Ocode wa kuwajengea miundombinu rafiki
ya ngazi itawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuweza kutembea kwa urahisi
zaidi kwenda madarasani.
Mkuu huyo, alibainisha kwamba, shirika la Ocode limeweza kuwa
mstari wa mbele katika kusaidia kwa hali na mali katika kuboresha sekta ya
elimu na kwamba msaada huo wa kuwajengea miundombinu ya ngazi kwa wanafunzi wa
shule hiyo, kutaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi ambao walikuwa
wanapata shida ya kupanda ili kuelekea madarasani.
“Katika shule yetu ya msingi ya Kibwegere kwa sasa tuna
wanafunzi 15 ambao wana mahitaji maalumu na kati yao waluvana wapo tisa
na wasichana wapo 6 hivyo kwa msaada huu wa shirika la Ocode la kujenga
miundombinu ya ngazi ni jambo ambalo litaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi
wetu kuweza kupita kwa urahisi kwani hapo awali walikuwa wanapata shida katika
suala zima la kupita”Alisema.
Mkuu huyo,katika hatua nyingine, alitoa pongeza kwa Shirika la
Ocode kwa kuweza kutoa msaada wa mambo mbalimbali katika shule hiyo ikiwemo
kuwajengea madarasa, kuwapatia viti na meza kwa walimu na wanafunzi lengo ikiwa
ni kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri na rafiki kwao.
Kwa upande wake, mmoja wa wakikilishi wa walezi wa watoto hao
wenye mahitaji maalumu amebainisha kwamba mjukuu wake anayetambulika kwa jina
la Mustafa Sefu mwenye umri wa miaka 10 alikuwa anakabiliwa na changamoto ya
viungo vya mikono na miguu lakini kwa sasa anaweza kutembea kutokana na msaada
wa vifaa ambao amepatiwa.
Hamza Miramboi ni Mwenyekiti wa miradi wa elimu katika manispaa
ya Ubungo, alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha kwamba wanaunga juhudi za
serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kwamba kwa sasa wanaendelea kutoa
misaada mbalimbali katika baadhi ya shule za msingi zilizopo Manispaa ya ubungo
ikiwemo kuwajengea uwezo wazazi,walezi na wanafunzi katika mfumo wa elimu
jumuishi.
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Ocode limekuwa likiunga
mkono juhudi za serikali kwa kipindi kirefu katika kuboresha sekta ya elimu
hasa katika shule mbalimbali zilizopo katika Manispaa ya Ubungo kwa kutoa vifaa
mbali mbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ikiwemo madawati, viti,
kujenga madarasa pamoja na kutoa elimu jumuishi.
No comments:
Post a Comment