KAMPUNI ZA SIMU ZATAKIWA KUFANYA TAFITI,KUTATUA KERO ZA MAWASILIANO KWA WANANCHI
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO,TEKNOLOJIA YA HABARI,MHANDISI ANDREA KUNDE(KUSHOTO) AKIWA NA KATIBU TAWALA WILAYA YA BAGAMOYO,KASILDA MGENI(KATIKAKATI),WA MWISHO KULIA NI MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE,RIDHIWANI KIKWETE,WAKATI ALIPOFANYA ZIARA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHALINZE.
NA VICTOR MASANGU, CHALINZENAIBU Waziri wa Mawasiliano
Teknolojia ya Habari Injinia Andrea Kundo, ameyaagiza
makampuni mbalimbali ya simu kuhakikisha wanaweka mipango ya kufanya utafiti wa
kina katika maeneo ambayo tayari yameweka uwekezaji wa kufunga mitambo ya
minara ili kuweza kubaini uhitaji wa
wananchi ikiwa ni kuwaondolea adha na usumbufu wa ukosefu wa mawasiliano
kwa wananchi.
Kauli hiyo,
ameitoa wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Chalinze iliyopo
Wilayani Bagamoyo, Mkoani Pwani, kwa ajili ya kuzungumza na watumishi pamoja na
mamlaka zinazohusika na mawasiliano ili kujadili changamoto mbalimbali zilizopo
na kuzifanyia kazi na kubioresha zaidi sekta ya mawasiliano.
Naibu Waziri
huyo, alisema kwamba nia kubwa ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha
kwamba inaboresha zaidi sekta ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali hapa
nchini, hivyo ni vema wadau wa masuala hayo wanapaswa kuweka mikakati yao
madhubuti ambayo itasaidia kuboresha mitambo yao ambayo wanaifunga ikiwemo
kwenda kuiangalia na kuifanyia ukarabati mara kwa mara ili iweze kufanya
kazi vizuri kulingana na mahitaji ya wananchi.
“Hapa kitu kikubwa napenda kuagiza kwamba makampuni haya ya simu inatakiwa sasa kuhakikisha wanafanya uwekezaji wao ambao unatija na kuwafikia wananchi katika maeneo husika lakini kikubwa zaidi ni kufanya utafiti wa maeneo husika hasa ili kutembelea minara ambayo inakuwa imefungwa kwa kipindi cha muda mrefu, lakini kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watuamiaji mitambo inashindwa kuwafikia wananchi katika maeneo mengine kwa hivyo ili ninaliomba sana,”aliongeza Naubi Waziri huyo.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameipongeza
serikali ya awamu ya tano kwa juhudi mbalimbali ambazo inazifanya lakini
amebainisha kwamba bado kuna baadhi ya vijiji katika jimbo lake kuna changamoto
ya upatikanaji wa mawasilano ya mtandao hivyo wananchi wanapata
shida sana katika suala zima la kuwasiliana.
Naye, Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Kasilda Mgeni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya Chalinze Ramadhani Posi waliongeza kuwa kumekuwepo na
baadhi ya madhara yatokanayo na ukosefu wa mawasiliano pindi
kunapoibuka sakata la migogoro ya wakulima na wafugaji inakuwa ni changamoto
kupata taarifa kwa wakati na kuomba waongezewe ruzuku katika suala zima la
mawasialino.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano, TCRA Kanda ya Mashariki, Mhandisi
Lawi Odiero, amebainisha kwamba lengo ambalo wamejiwekea ni
kuhakikisha wanalinda na kuboresha sekta ya mawasiliano kwa kuzingatia sheria,
taratibu na miongozo mbali mbali ambayo imetolewa inafutwa bilaya kuvunjwa nia
ikiwa ni kuhakikisha kwamba huduma na hiyo inaleta mabadiliko chanya.
“Kwa
sasa mabadiliko katika sekta hii kwa kweli yameleta mabadiliko makubwa sana na
kuweza kurahisisha na kubadili hata kasi ya maendeleo kutokana na kuendesha na
kufanya shughui zetu za kuwasiliana hivyo kumesaidia kuongeza tija zaidi katika
mambo mengine hata ya kubadilisha kasi ya maendeleo kwa wananchi wetu wa
Tanzania,”alibainisha Mhandisi Odiero.
Kadhalika,
aliongeza kuwa kwa sasa, TCRA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa vyombo
vya habari, itawasaidia kwa hali na mali katika kuwapa miongozo mbalimbali
ambayo itawasaidia kufungua redio mbalimbali za kijamiii ambazo zitakuwa
zikitumika katika kuwafikishia ujumbe mbalimbali juu ya shughuli za kimaendeleo
ambazo zinafanyika katika maeneo yao.
No comments:
Post a Comment