Breaking News

Jul 5, 2021

TEKNOLOJIA YA KICHINA YAWANUFAISHA WAKULIMA WADOGOWAGODO MOROGORO

TEKNOLOJIA YA KICHINA YAWANUFAISHA WAKULIMA WADOGOWAGODO MOROGORO

Na Thadei Hafigwa                                                                                           

MRADI wa maendeleo ya teknolojia za kilimo na mifugo chini ya ufadhili wa serikali ya Tanzania na serikali ya china imeleta mafanikio kwa wakulima wadogowadogo wa mazao ya mahindi na mpunga mkoani Morogoro.

Mratibu wa Mradi huo,Ernest Mkongo amebainisha hayo wakati wa ziara ya mafunzo Mkoani Morogoro kwa wanafunzi wakitanzania wa masafa, kutoka chuo Kikuu cha Kilimo cha China (China Agriculture University).

 Mkongo amesema mradi huo umeleta tija kwa wakulima wa vijiji vya Peapea,mtego wa simba, kwa kipindi cha miaka miwili ya awali hali toka mwaka 2014,ambapo wakulima wa vijiji hivyo waliweza kupata mafanikio ya mavuno kutoka magunia manne ya mahindi kwa hekari moja hadi magunia 16.

“baada ya mafanikio hayo ya mradi wa maendeleo ya teknolojia ya Kilimo na mifugo kuwa wenye manufaa kwa wakulima wadogowadogo eneo la mradi ulipanuliwa kutoka vijiji viwili vya awali na kuogeza vijiji vingine vinane.”Alisema Mkongo.

Aidha,Mkongo alisema kuwa mradi wa kijiji cha  Mtego wa simba, ulihusisha maendeleo ya vyuo vikuu,chuo kikuu cha kilimo cha china,chuo kikuu cha sokoine cha Kilimo(SUA), serikali ya mkoa wa Morogoro ili wakulima waweze kunufaika kwa kubadilisha maisha ya wananchi vijijini kupitia sekta ya kilimo chenye tija katika mfumo wa nguvukazi.


Kwa upande wake,Afisa Kilimo mwandamizi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Gambishi 
Evance  alisema lengo kuu  la mradi ilikuwa kukuza ukuaji wa uchumi kwa kukuza, kuanzisha 
na kusambaza teknolojia za kilimo na mifugo kupitia uzoefu wa Wachina katika
 kupunguza umaskini. 

Alifafanua kuwa mradi wa upanuzi wa vijiji 8, ulizinduliwa Machi 2018, vilivyopo katika Wilaya 7 za mkoa wa Morogoro, Vijiji hivyo ni Letugunya na Ngayaki katika halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Kitete katika Kilosa, Kisegese katika Halmshauri ya Wilaya ya Kilombero, Kiswago katika Malinyi DC na Kijiji cha  Kikundi halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.

Maeneo mengine ya mradi alitaja ni Makuyu katika Wilaya ya Mvomero na Kijiji cha Mwaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga. Mradi huu unakusudia kufikia angalau wakulima 1,667 kila mmoja akiwa na angalau ekari moja ya shamba la mahindi.

Julieth Gasper ni miongoni mwa wanafunzi wa chuo kikuu cha China walioshiriki katika ziara hiyo ya mafunzo,aliongea kwa niaba ya wenzake alisema kuwa wao wakiwa wanafunzi wameguswa kwa namna ya pekee kwa jinsi serikali ilivyoweza kujali masilahi ya wakulima wadogowadogo waliopo vijijini.

Hata hivyo,Julieth hakusita kushauri serikali na wadau wake wa maendeleo waangalie namna ya kuwarahisishia wakulima kupata teknolojia rahisi itakayowarahisishia kushughuli zao za ulizalishaji wao  ili kilimo chenye tija kiwe endelevu.

 

 


No comments:

Post a Comment