SERIKALI YAWEKA MPANGO ENDELEVU WA
UPIMAJI ARDHI.
Na
Lilian Lucas Morogoro
KATIKA kipindi cha miaka
mitano ijayo Serikali imelenga kupima takribani asilimia 37 ya ardhi kwa ajili
ya uwekezaji, makazi, biashara na matumizi mengine ya ardhi.
Waziri
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, William Lukuvi alisema hayo juzi mjini Morogoro katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu mkuu wa
wizara hiyo,Mary Makondo, kwenye
uzinduzi wa Kongamano la Kitaifa la masuala ya Ardhi katika kuadhimisha
miaka 20 ya utekelezaji wa sheria za ardhi nchini.
Kongamano
hilo, lililoshirikisha washiriki kutoka Taasisi za Umoja wa Mataifa, washirika
wa maendeleo na Asazi za Kiraia na Sekta Binafsi lilikuwa na Kauli mbiu ; Utekelezaji thabiti
wa sheria za ardhi ni msingi wa usalama
wa milki za ardhi kwa wananchi katika
kufikia Maendeleo Endelevu”.
Waziri Lukuvi alisema, lengo hilo litafikiwa
kwa kutekeelza miradi mbalimbali katika mamlaka za upangaji kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za
Mita na wadau wengine.
Lukuvi
alisema, licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha kila kipande cha
ardhi kinapangwa, kupimwa na kumilikishwa
na wananchi kuwa na milki salama , kwa sasa ni asilimia
takribani 25 ya ardhi ambayo imepangwa , kupimwa na kulimilishwa.
Lukuvi
alisema, hali hiyo inachangiwa na uhaba wa rasilimali fedha na ukubwa wa nchi
yetu inayotakiwa kupimwa na kumilikishwa .
“Tanzania
ni moja wapo ya nchi kubwa Barani Afrika
na hivyo, imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha kila kiande cha
ardhi kinapangwa , kupimwa na kumilikishwa ambayo ndiyo suluhusho la kudhibiti
migogoro ya matumuzi ya ardhi isiendelee kujitokeza “ alisema Lukuvi.
Kwa
upande wa udhibiti wa migogoro ya
matumizi ya ardhi, Waziri alisema Serikali chini ya wizara hiyo inaendelea
kutatua migogoro na kero mbalimbali za wananchi kwa njia mbalimbali ikiwemo ya Programu ya Funguka kwa Waziri ambayo
imeweka utaratibu wa kufanya mikutano mbalimbali na wananchi wenye kero au
changamoto zinazohusiana na sekta ya ardhi maeneo mbalimbali nchini na kuzipatia
ufumbuzi wa papo kwa hapo.
Waziri
pia alitumia fursa hiyo kuipongeza Tanzania Land Alliance (TALA) kwa kubuni na
kufabnikisha kongamano hilo ambalo lilioenga kujadili masuala mbalimbali
yanayohusu haki za ardhi za wazalishaji wadogo.
Naye,
Mratibu wa TALA, Bernard Baha, katika taarifa yake alisema, Jukwaa hilo
limewezesha kutoa elimu kwa wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji katika kutambua haki za kisheria na wajibu wao
wa umiliki wa ardhi nchini .
Kwa
upande wake Profesa Issa Shivji, akiwasilisha mada ya masuala ya ardhi na
mustakabali wa haki za ardhi za wazalishaji wadogo kwa njia ya mtandao alisema,
siku hizi mchakato wa umilikishwaji wa ardhi umepamba moto na lengo la Wizara
yenye dhamana ni kuona maendeleo yanapatokana kupitia ardhi iliyopo na kutaka
elimu zaidi itolewa kwa wananchi hasa wa
vijijini.
Kwa
upande uzalishaji wa mazao, alisema, kilimo cha wakulima wadogo bado
hakina tija kwa vile hawajawekewa mazingira rafiki yanayowezesha wazalishe kwa tija tofauti na kilimo cha
wakulima wakubwa chenye tija kwa kuwa wao wamewekewa mazingira mazuri katika uzalishaji.
No comments:
Post a Comment