CHANGAMOTO YA AJIRA TANZANIA VIJANA 65,000 WAFIKIWA ILI KUKUZA UJUZI
Na.Lilian
Lucas,Moogoro
KUTOKANA na kuwepo kwa
Changamoto ya ajira Serikali ya Tanzania imeweza kuwafikia vijana zaidi ya
65,000 kwa kuwawezesha kukuza ujuzi ili waweze kuajirika na kujiajiri wenyewe.
Afisa
Maendeleo ya Vijana, Uratibu, na Uwezeshaji vijana kiuchumi toka ofisi ya
Waziri Mkuu Nassibu Mwaifunga alisema hayo wakati wa Kikao cha wadau wa mradi
wa mabadiliko katika Sekta ya Ajira kwa Manufaa ya Jamii Afrika Mashariki (TESCEA)
kupitia Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Mwaifunga
alisema tatizo la ajira limekuwa likiwalenga hasa vijana na kila mwaka kupitia
program ya Ukuzaji Ujuzi kwa watanzania (SDL) imekuwa ikiwafadhili vijana zaidi
ya 5,000 na wamekuwa wakinufaika na serikali imekuwa ikifanya hivyo kwa mujibu
wa waajiri wa makapuni na taasisi za serikali na nyingine za binafsi wanaleta
mahitaji yao ya vijana wenye sifa na ujuzi wanaoutaka na kupatiwa.
“Ili
kuhakikisha vijana wanakuwa na maarifa na ujuzi wa kisasa kukabiliana na
changamoto ya ajira Serikali imekuwa ikiratibu program ya utambuzi wa ujuzi
uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa maana ya kuwapa kozi ya muda mfupi
kwa lengo la kuziba pengo la ajira,”alisema.
Alisema,
kimsingi Serekali inaendelea kutenga na kuwahudumia vijana kwa sababu ni kundi
kubwa wanahitajika, na Chuo Kikuu Mzumbe kimekuwa mstari wa mbele hususani kwa
namna kinavyotoa maarifa kwa vijana wahitimu kwa lengo la kuwaandaa kuingia na
kushindana kwenye soko la ajira.
Mratibu
wa jukwaa la wadau wa Mradi, Musali Milanzi toka Mzumbe alisema kama chuo
wamekuwa wakiwaongezea uwezo waalimu wa kufundisha wanafunzi na kubadili mbinu
za ufundishaji na kuangalia mitaala itakayoendana na mahitaji ya soko.
Pia,
Milanzi alisema mradi una lengo la kukuza na kuwajibika kwa wanafunzi na hatua
ambazo zitawafanya kuweza kuajirika kwa upande wa sekta binafsi, Serikali na
hata kutengeneza wenyewe ajira zao.
Mwanafunzi
Samuel Elisha, alisema kuwepo kwa mradi kama huo unawawezesha kusaidia
kuzalisha wanafuzni ambao wanakuwa na ujuzi wa kufikiria mbali tofuti na
ilivyokuwa zamani na wamekuwa wakijijengeana uwezo wa kujiamini kuwa
wanapomaliza masomo wasitegemee ajira ya kuajiliwa moja kwa moja na badala yake
wawe na uwezo wa jiajiri pia.
No comments:
Post a Comment