VYAMA VYA USHIRIKA
VYATAKIWA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA HUDUMA ZA FEDHA
Na
Lilian Lucas,Morogoro.
Vikundi
vya Ushirika vinavyojihusisha kuweka akiba na kukopeshana Vimetahadharishwa na
kutakiwa kusajili vyama vyao kwenye mfumo kwa mujibu wa sheria ndogo ya huduma
za fedha namba 10 ya mwaka 2018 ili kuendesha shughuli zao kwa weledi.
Aidha,
wameelezwa kuwa bila kufanya hivyo vitakuwa kwenye hatari ya kukamatwa kwa
makosa ya utakatishaji fedha au uhujumu uchumi.
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shighela, alisema hayo wakati akizindua jukwaa la
kwanza la ushirika kwa mkoani hapa lililohusisha wanaushirika wawakilishi
kutoka vyama mbalimbali vya ushirika ikiwemo ushirika wa mazao, ushirika wa
kuweka na kukopa, ushirika wa viwanda, walaji, ufugaji, miradi ya pamoja,
huduma na wengine.
Shigela
alisema kumekuwa na vyama vingi vya ushirika lakini havifuati sheria, kanuni
wala taratibu na pindi vinapopata tatizo kusaidia inakuwa shida.
“Uwepo
wa ushirika wenye kufuta sheria serikali kunasaidia kupata mikopo na mitaji kwa
urahisi kutoka kwenye taasisi na asasi za kifedha,”alisema mkuu huyo wa mkoa.
Pia, Shigela alionyesha masikitiko kwa namna vyama vya ushirika vinavyotambuliwa kutokuwa na maghala ya kuhifadhi mazao ya wakulima na yote yaliyopo ni ya watu binafsi, hivyo aliwataka warajisi wa vyama vya ushirika wa wilaya na mkoa kuanza safari ya kuhakikisha vyama vya msingi hasa vya mazao kunaanza mchakato wa kujenga maghara.
Alisema,
kukiwa na maghara kutakuwa na uhakika wa vyama kuwa na takwimu sahihi juu ya
uzalishaji katika vijiji na wilaya, kupata wanunuzi wengi na wa uhakikia,
wananchi watapunguza upotevu wa mazao wanayovuna, kwani wengu upoteza mazao yao
kutokana na kutokuwa na kukosa maeneo ya kuhifadhi wengi wanahifahdi nje na
pale panapotokea mabadiliko ya tabia nchi baadhi ya mazao upotea kutokana na
Mvua zinazonyesha.
“Tuangalie
vyama viko maeneo gani, vinafanya shughuli gani, vina wanachama kiasi gani, na
je vinapotaka kuwasaidia wakulima kwenye masoko vinatumia utaratibu gani na
vinahifadhi sehemu moja ama kwa kutumia maghara ya watu binafsi ama wanunuzi wanashindanishwaje,”alielekeza.
Mwenyekiti
wa jukwaa la ushirika mkoa wa morogoro, Iddi Bilali,alisema hadi sasa jumla ya
vyama 60 vimeomba leseni kwenye mfumo na kati yake 21 vimeshapata huku 39
vikisubiri mchakato toka tume ya maendeleo ya ushirika.
Bilali,
alibainisha changamoto zilizopo katika ushirika kuwa ni makato toka kwa
waajiri, mchakato wa upatikanaji wa leseni ambayo uchukua muda mrefu, pamoja na
kodi ya mapato, kodi ya shikizo na kodi ya ardhi.
Mkuu
wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando akatahadharisha viongozi na kuwataka
wanaushirika kuheshimu sheria na kuondokana na ubadhirifu kwenye maeneo yao ya
kazi.
Naye,
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro, Kenneth Shemdoe licha
ya kubainisha ukosefu wa mfumo mzuri na wa uhakika wa uuzaji mazao, alieleza
namna ofisi hiyo ilivyofanikisha utatuzi wa migogoro ambayo mingi alisema ni ya
kurithi kutokana na awali vyama vingi kuendeshwa kinyume na sheria.
Aidha,
alisema pamoja na mkoa kuwa na vyama vya ushirika vya mazao zaidi ya 239,
migogoro iliyotatuliwa ni 50 na wameendelela kutoa elimu ya ushirika, akiba na
kukopa kwa vyama nia ikiwa ni kuendelea kupunguza migororo hiyo.
No comments:
Post a Comment