MKUU WA
WILAYA BAGAMOYO, ZAINABU ISSA WA KATIKATI AKIPOKEA MAELEKEZO KUTOKA KWA
MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA CHALINZE, RAMADHANI POSSI WA KULIA WAKATI
WA ZIARA MAALUMU KWA AJILI YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MBALI MBALI YA
MAENDELEO AMBAYO INATARAJIWA KUPITIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2021
KUSHOTO KWAKE NI KATIBU TAWALA WA WILAYA HIYO KASILDA MGENI.
VICTOR MASANGU,
BAGAMOYO
MKUU
wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Issa, amewaonya vijan na kuwataka
kuachana kabisa na vitendo vya matumizi ya madawa ya kulevya ambavyo vimekuwa
vikipelekea baadhi ya vijana kupoteza nguvu kazi ya taifa na
kuahidi kulivalia njuga suala hilo kwa kuwashirikisha
kuwapatia vijana hao fursa mbali mbali zilizopo kwa lengo la
kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.
Hayo
ameyabainisha wakati ziara maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya kupitia miradi
mbalimbali itakayopitiwa na mbio za mwenge wa uhuru wa mwaka 2021 ambapo
ilijumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ya Wilaya nzima ya Bagamoyo
wakiwemo wakurugenzi, wakuu wa idara, pamoja na kamati ya ulinzi na
usalama lengo ikiwa ni kujionea mwenendo mzima sambamba na kutoa mapendekezo
yao.
Katika ziara
hiyo, Mkuu huyo alipokuwa katika mradi wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya
ambao upo katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo aliweza kuwatembelea
vijana hao na kuwaasa kuachana kabisa na vitendo hivyo vya matumizi ya madawa
ya kulevya na kwamba wanatakiwa kujirekebisha na kujikita zaidi katika
kushiriki kikamilifu katika shughuli mbali mbali za uzalishaji mali.
“Mimi
kama mkuu wa Wilaya mpya ya Bagamoyo nimekuja hapa kuwatembelea na
kujitambulisha kwenu lakini kitu kikubwa ninawaomba sana kubadilika na suala la
matumizi ya madawa ya kulevya ni hatari sana kwa afya yenu na kwamba
kufanya hivyo kunasababisha madhara makubwa na pia kunapelekea kwa kiasi
kikubwa kutpoteza nguvu kazi ya Taifa hivyo ombi langu hili ninawaomba
sana mlifanyia kazi vijana wa Bagamoyo ,”alisema Mku huyo.
Aidha,
amewataka vijana hao ambao hapo awali walikuwa wamejiingia katika matumizi ya
madawa ya kulevya kuhakikisha wanazingatia maelekezo yote ambayo wanapatiwa na
wataalamu wa afya na kwamba atakuwa nao bega kwa bega katika kuwasaidia
kuwainua kiuchumi kupitia fursa mbali mbali amabzo zitakuwa zikijitokeza.
Akiwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, aliupongeza uongozi huo kwa kutekeleza
agizo la serikali kwa kuweka mfumo mzuri wa ukusanyaji wa mapato na
kwamba ana imani kwamba utaweza kusaidia zaidi katika suala zima la kuongeza
kipato na kuwataka waendelee na mfumo huo ili kuthibiti wizi la wizi wa fedha .
Kadhalika,
aliwataka kuhakikisha wanajiwekea utaratibu mzuri hospitalini hapo wa
kuhakikisha wanashughulikia chagamoto ya ukosefu wa madawa kwa lengo la
kuwawezesha wananchi kupata huduma ya matibabu kwa uhakika.
“Nimeweza
kujionea jinsi ya mfumo wa makusanyo ya mapato katika Hospitali hii ya Wilaya
ya Bagamoyo na kimsingi ameupongeza uongozi kwa kazi nzuri ambayo
ambao wameifanya na kwamba waendelee kujitahidi zaidi katika
kuboresha sekta ya afya na kwamba serikali ya awamu ya sita itaendelea kuongeza
kasi zaidi katika huduma ya afya,”alisema Mkuu huyo.
MWONEKANO WA MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO,ZAINABU ISSA,(ALIYEVAA VAZI LA KUJITANDA) AKIWA PAMOJA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI YA WILAYA PAMOJA NA WAKUU WA IDARA WAKATI WALIPOTEMBELEA NA KUJIAONEA MRADI WA UJENZI WA BARABARA ROUND ABOUT ILIYOPO ENEO LA CHALINZE.
Katika hatua
nyingine, Mkuu huyo aliwaataka watumishi wa halmashauri zote mbili za Bagamoyo
na Chalinze kufanya kazi kwa kuzingatia sharia na taratibu zote na kwamba
wasimamie miradi mbali mbali ya maendeleo kwa maslahi ya wanachi na Taifa kwa
ujumla.
Naye,
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Kasilda Mgeni ameahidi
kuyafanyia kazi yale yote ambayo yameelekezwa na Mkuu wa Wilaya na kubainisha
kwamba atashirikiana bega kwa began na watumishi wenzake katika kusikiliza kero
na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi wa
kudumu.
Nao baadhi
ya vijana ambao wameachana na matumizi ya madawa ya kulevya,Fasto Fikiri na
Shukuru Mohamed wamemshukuru na kutoa pongezi zao za dhati kwa Mkuu huyo mpya
kwa kwenda kuwatembelea na kuwaasa na madawa ya kulevya na kwamba wameahidi
kutojiingiza tena katika matumizi hayo na kutumiza fursa zilizopo katika kuleta
mabadiliko chanya ya kiuchumi.
Katika
ziara hiyo, wajumbe waliweza kutembelea na kukagua zaidi ya miradi 15 ya
ikiwemo ujenzi wa restaurant ya msolwa, mapamabano dhidi ya rushwa,ujenzi wa
barabara ya round about chalinze, ujenzi wa tanki la maji safi Mboga,ujenzi wa
zahanati ya kihangaiko,mapambano dhidi ya ukimwi,shamba la kilimo cha mboga
mboga,ujenzi wa chumba cha maabara,ujenzi wa soka la kisasa la samaki,pamoja na
mapambano ya madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment