MBUNGE VITI MAALUM PWANI ATOA MIFUKO 100 YA SARUJI KWA SHULE MSINGI,SEKONDARI
NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika
kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu, Mbunge wa viti maalumu
Mkoa wa Pwani kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hawa Mchafu ameamua
kuchangia mifuko 100 ya sarufi katika kata mbili za Tengeleni na Kipalang’anda
kwa lengo la kuboresha sekta ya elimu kwa shule za msingi pamoja na sekondari.
Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji katika hafla fupi ambayo
ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi katika ngazi za kata
wilaya,na Mkoa akiwemo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani, Mbunge huyo
alibainisha kwamba ametoa mifuko 50 katika kata ya Tengeleni na mifuko
mingine 50 katika kata ya Kipalang’anda ambayo itasaidia katika mradi wa ujenzi
wa shule mpya ya sekondari sambamba na kufanya ukarabati katika shule ya msingi
msingi ya vikangara ya shinikizi.
Mchafu aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita
ambayo inaongozwa na Rais Mama Samia Suluhu ni kuendeleza zaidi kuboresha sekta
ya elimu hivyo ameamua kusapoti elimu kwa lengo la kuwaondolea changamoto mbali
mbali ambazo zilikuwa zikiwakabili wanafunzi kutembea umbari mrefu na baadhi ya
kusoma katika mazingira ambayo sio rafiki.
“Kimsingi ndungu zangu nimekuja Wilayani Mkuranga na
ninashukuru nimepokelewa vizuri na Mkuu wa Wilaya na lengo langu kubwa ni kuja
kutekeleza ilani ya chama sambamba na ahadi zangu nilizozitoa wakati wa
kampeni kwa hiyo nimetoa mifuko hii 100 ya sarufi ambayo itagawanywa katika
kata hizo mbili pamoja na kuja kuwapa mrejesho kwa kile ambacho tumekijadili
katika kipindi chote cha bunge letu la bajeti la mwaka huu ili mjone jinsi
serikali ya awamu ya tano ilivyojipanga katika kuleta maendeleo kwa
wananchi,”alisema Mchafu.
Katika hatua nyingine, Mchafua aliwaahidi wananchi wa
Mkurunga kuendelea kushirikiana bega kwa bega katika kusikiliza kero na
changamoto ambazo zinawakabili na kwamba waendelee kumwombea Rais wa
awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan.
Awali, Mkuu mpya wa Wilaya ya Mkuranga, Hadija Ally
amefarijika na ujio wa Mbunge huyo
kufanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya yake na kuchangia mifuko 100 ya
sarufi kwa lengo la kukabilian na changamoto za miundombinu zilizopo
katika shule za msingi na sekondari.
“Kwa kweli huyo Mbunge wetu wa viti maalumu Mkoa wa Pwani tumetoka naye mbali sana naweza kusema anajituma sana katika kutekeleza majukumu yake kwa vitendo na mimi ni mwalimu wangu mzuri sana na katika hili nimpongeze sana maana katika Mkoa wa Pwani mmepata bahati ya kupata jembe kweli kweli na mkimtumia vizuri atakuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa wananchi.”alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa wanawake (UWT) ya Chama
cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani Farida Mgomi aliwaeleza wananchi kwamba
lengo lao kubwa ni kuwaletea maendeleo na kwamba yale yote ambayo yanafanyika
ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho na kutumia fursa hiyo kumpongeza kwa
dhati Mbunge Hawa Mchafu kwa kuweza kufanikiwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo
lengo ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo.
Naye Diwani wa Kata ya Tengelea Shabani Manda
alibainisha kuwa juhudi kubwa ambazo amezifanya Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa
Pwani zitaweza kusaidia na kuleta mabadiliko chnaya ya kimaendeleo na kwamba
sapoti hiyo ya mifuko 50 waliyopatiwa itakwenda kufanya ukarabati
katikamadarasa ambayo wanasomea wanafunzi wa shule ya msingi shikizi ya
Vikangara ili wanafunzi hao wameze kusoma kaatika mazingira ambayo ni rafiki.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kipalang’anda Shomari
Mwambala amempongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi zake alizozitoa kwa
wananchi kwa vitendo na kwamba mifuko hiyo ya sarufi itaweza kusaidia kwa kiasi
kikubwa katika kuanza harakati za mradi wa ujenzi huo wa shule ya sekondari na
kuwaondolea adha wanafunzi wa kutembea umbari mrefu.
Kadhalika, aliongeza kuwa kwa sasa tayari wameshatenga eneo
lenye ukumbwa wa hekari zipatazo nane kwa ajili ya kuanza mradi wa ujenzi huo
na kwamba kutahitajika nguvu zingine za zihada kutoka serikalini pamoja na
wadau wengine mbali mbali wa maendeleo ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea
katika suala zima ya kuboresha elimu.
No comments:
Post a Comment