MBUNGE VITI MAALUM
PWANI AWAGEUKIA WALIMU,ATOA SARUJI MIFUKO 50
NA
VICTOR MASANGU, KIBAHA
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa
wa Pwani (CCM) Hawa Mchafu amechangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya mradi wa ujenzi
wa jengo la utawala katika shule ya sekondari Pangani, iliyopo Wilayani
Kibaha, Mkoani Pwani kwa lengo la kuwakomboa walimu na kuwaondolea changamoto
ya ukosefu wa ofisi ambayo kwa sasa inawapelekea kuendeshea shughuli zao
za kikazi katika madarasa ya wanafunzi.
Mchafu
mbali na kutoa msaada huo wa mifuko ya saruji katika shule hiyo akiwa
katika ziara yake ya Kikazi Wilayani Kibaha aliweza pia kuchangia mifuko 30
kwa ajili ya ujenzi wa duka la wakinamama wajarisiamali wa UWT ili
waweze kupata fursa mbali mbali za kuuzia bidhaa zao ambazo wanazozizalisha na
kupata masoko kwa urahisi.
Katika ziara
yake hiyo ya kikazi aliambatana na baadhi ya viongozi wa chama cha
mapinduzi pamoja na na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya UWT kwa lengo la
kuweza kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo na kutoa msada wa
mifuko ya saruji mchanga ikiwemo kusikiliza kero mbali mbali wanazokabiliana
nazo na kuzitafutia ufumbuzi na kuwapatia mrejesho juu ya kile ambacho
wamekizungumza bungeni katika bajeti ya mwaka huu.
“Ndugu
zangu nimeamua kufanya ziara yangu hii ya kikazi ambayo nitapita katika maeneo
mbalimbali ambapo nimeweza kuchangia mifuko 50 ya saruji katika shule ya sekondari
pangani itasaidia katika ujenzi wa mradi wa jengo la utawala,”alisema Mchafu
Pia,Mchafu
aliongeza kuwa serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais Mama Samia
Suluhu Hassan lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya elimu
na kutengeneza mazingira ya kujijisomoa kwa wanafunzi pamoja na kufundishia
walimu hivyo ndio maana ameona kuna umuhimu wa kusaidia katika suala la elimu.
Kadhalika
aliwahimiza walimu hao wa shule ya Pngani kuhakikisha wanafundisha kwa bidii na
kuweka mikakati madhubuti ya kujipanga katika kuongeza kasi ya ufaulu kwa
wanafunzi ili siku moja shule ya Pnagani iweze kuwa katika ramani ya kufanya
vizuri katika mitihani mbali mbali ikiwemo ile mitihani ya ngazi ya Taifa.
Katika
hatua nyingine mbunge huyo aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa
kushirikiana bega kwa began a viongozi wa chama wa serikali pamoja na wananchi
katika kushiriki mambo mbali mbali ya kimaendeleo na kwamba ataweka utaratibu
wa kusikiliza kero na changamoto ambazomzinawakabili ili kuzichukua na kwenda
kusisemea pindi anapokuwa katika vikao vya bunge.
Naye
kaimu Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Pangani Diksoni Martini
alimpongeza Mbunge Mchafu kwa hatua hiyo ya kwenda kufanya ziaara katika eneo
lao na kuwapatia mifuko hiyo 50 ya saruji amabayo kwa upannde wao itakuwa ni
mkombozi mkubwa wa kumaliza changamoto hiyo ya kutokuwa na jingo la utawala
kwani kwa kipindi hiki wamekuwa wakifanya kazi zao katika mazingira amnbayo sio
rafiki sana.
“Mimi
kama Kaimu Mkuu wa shule hii ya sekondari Pnagani natoa shukrani zangu za
kipekee zaidi kwa Mbunge wa viti maalumu hawa Mchafu kwa kuweza kutushika mkono
kwa kutuchangia mifuko hii ya saruji kwa kweli shule ambayo ilianzishwa mwaka
2007 kwa sasa wanafunzi wanasoma darasa moja katika mlundikano mkubwa sana na
wakati mwingine darsa moja wanasomo wakiwa idadi yao ni 100 kwa hivyo bado tuna
upungufu wa madarasa kama sita vile,”alisema Mkuu huyo.
Mwenyekiti
wa UWT katika halmashauri ya mji Kibaha Elina Mgonja alieleza kuwa lengo
kubwa la wanawake wajasiriamali ni kujikwamua kiuchumi hivyo msaada huo
walioupata kutoka kwa Mbunge kwa ajili ya ujenzi wa duka la kuuza bidhaa zao
utakuwa ni mkombozi mkubwa kutokana na kupata sehemu rasmi ambayo watakuwa
wanaitumia katika kuuzia bidhaa zao mbali mbali ambazowanazizalisha wao
wenyewe.
Naye Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Selena Wilsoni aliongeza kuwa uwepo wa
kuanzishwa kwa mradi huo kwa wanawake wa UWT kibaha mji ni moja ya hatua kubwa
ya kujileteaa maendeleo na kwamba atahakikisha kwmaba analisimamia suala hilo
ipasavyo na kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuondokana na
wimbi la
umasikini.
No comments:
Post a Comment