Breaking News

Oct 18, 2020

MGOMBEA UDIWANI TUNGI KUENDELEZA SEKTA YA SANAA,MICHEZO KUWAPEKA 'VYUONI'

 Mgombea nafasi ya udiwani Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro, Nimala Mchunguzi akinadi ilani ya chama chake kwa wananchi(hawapo pichani)

Na Severin Blasio

MGOMBEA udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro Nimala Mchunguzi amesema akipewa ridhaa na wananchi kuwa diwani wa kata hiyo atawapeleka wasanii na wachezaji kwenye vyuo ili waweze kufanya vizuri katika ushindani.

Aidha akinamama,mafundi na waendesha pikipiki`bodaboda`nao wametakiwa kujiunga katika vikundi  ili waweze kusaidiwa mikopo.

Mchunguzi alizungumza hayo alipokutana na makundi ya wasanii,wajasiriamali  na wanamichezo waliopo katika kata hiyo kwa ajili ya kuomba kura za Udiwani ,Ubunge na Uras.

“Mkinipa ridhaa ya kuwa diwani wenu nimepanga wasanii niwapeleke kwenye vyuo vya sanaa na mziki…Sijaomba udiwani kwa ajili ya kula bali kuwainua wasanii na wanamchezo wafanye vyema.

“Nataka wanamichezo na wasanii  wa kata ya Tungi wawe wanashindania zawadi kubwa kama vile mbuzi na ng'ombe badala ya kushindania zawadi ndogondogo ka vile kuku.

"kwa akinamama wajasiriamali ,na waendesha bodaboda anzeni kujiunga kwenye vikundi ili nikiapishwa nianze na niyi kuwapa mikopo.”alisema Mchunguzi.

Alisema anahitaji kuweka heshima kwa wasanii na wanamichezo wa Tungi wajiwezeshe kuepuka ombaoba wanapopata mechi na kushauri kuunganisha nguvu kwa kila timu ili iwe rahisi kuwasaidia.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wasanii wa singeli hipop na wanamichezo wa kareti na mpira wa miguuna pete

 

No comments:

Post a Comment