Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzana Raymond akitoa taarifa kwa waandishi
wa habari ya kipindi cha kuanzia mwezi wa kuanzia Julai hadi
Septema mwaka huu wa 20202.
VICTOR
MASANGU, PWANI
TAASISI ya kuzuia na na rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuokoa mali na kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia mbili katika kipindi cha robo ya tatu kuanzia mwezi wa Julai mpaka Septemba mwaka 2020 kutokana na kushughulikia malalamiko mbali mbali yaliyofanyiwa uchunguzi na kazi.
Akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Raymond alisema
kwamba ofisi yake katika kipindi hiki cha robo ya tatu ilipokea malalamiko 318
ambayo kati ya hayo malalamiko 157 unaendelea kufanyiwa kazi katika hatua mbali
mbali na malalamiko 74 yalionekana kuangukia katika sheria nyinginezo.
Mkuu huyo alisema kwamba katika
kipindi hicho jumla ya kesi 10 zilitolewa hukumu na upande wa wa jamhuri
ulifanikiwa kushinda kesi zipatazo 6 kwa washitakiwa kuamuliwa kufungwa jela na
wengine kuamuliwa kulipia faini ambapo kesi nne watuhumiwa hawakukutwa na
hatia na hivyo waliweza kuachiwa huru.
Mmoja wa maafisa wa taasisis ya kuzuia na
kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Pwani Fredrick Mbigili akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa kutoa taarifa ya
robo mwaka kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu.
Pia Mkuu huyo akizungumzia
kuhusiana na halmashauri ya Chalinze iliweza kufanikiwa kurejesha kiasi cha
zaidi ya shilingi milioni 6 ambazo zilitokana na ukiukwaji wa taratibu za
mikopo ambayo inatolewa kwa vikundi vya wanawake vijana pamoja na makundi ya
watu wenye ulemavu uliofanywa na kikundi cha Miono Saccos kilichopo kata ya
miono.
“Katika uchukuzi wetu ambao
tulioufanya sisi kama takukuru Mkoa wa Pwani tulibaini kamba viongozi wa
kikundi hicho cha miono Saccos yaani Mwenyekiti na katibu wake walipokea mkopo
usio kuwa na riba kutoka kwa halmashauri ya chalinze na wao kuamua kwenda
kukopesha kwa wafanyabiashara pasipo hata kuwajulisha wahusika ambao ni wana
vikundi,”alisema Suzana.
Kadhalika akifafanua kuhusiana
na mafanikio ambayo iliyapata ofisi ya Takukuru Kibaha iliweza kufanikiwa
kurejesha nyumba ya iliyokuwa ikimilikiwa na Bi. Mayasa Ally iliyokuwa
ikishikiliwa na kutaka kuuzwa na Godlisten Ndimbo kinyume kabisa na sheria na
taratibu kutoka na madai ya kushindwa kumaliza deni alilokuwa akidaiwa.
Akizungumza zaidi kuhusiana na
Ofisi ya Takukuru Wilaya ya Mafia yenyewe katika kipindi hicho iliweza kuokoa
kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 4 ambazo zilikusudiwa kuchepushwa na
baadhi ya watumishi na mawakala ambao wanafanya kazi katika halmashauri ya
Mafia ambao wana dhamana ya kukusanya ushuru kwa kutumia mashine ya kieletroniki.
Pia Suzan alifafanua kuwa
katika Wilaya ya Kibiti waliweza kuokoa bati zipatazo 168 zenye thamani ya
kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 4 zilizotakiwa kuezekwa katika
madarasa ya shule ya msingi Nyambagala iliyopo kata ya Dimani Wilayani Kibiti
ambapo awali ilibainika kuwa mkataba huo wa ujenzi wa madarasa hayo
kuezeka mabati ya ukumbwa wa gaige 28 kinyume na makubaliano.
Akifafanua zaidi Mkuu huyo wa
Takukuru alieleza kwamba katika Wilaya ya Kibiti waliweza kupambana vilivyo na
kufanikiwa kuokoa kisi cha shilingi milioni mbili na nusu kutokana na tozo
mbali mbali za kodi kutoka kwa wafanyabiashara wa zao la misitu kwa kuvuna
magogo ya miti aina ya mkuruti katika maeneao yasiyoruhusiwa.
Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa upande wa Wilaya ya Kisarawe waliweza kumsaidia mwananchi mmoja aliyejulikana kwa jina la Khadija Bani mkazi wa mtaa wa Bomani kulipwa kiais cha shilingi 12 na laki tano kutokana na kuchukuliwa shamba lake na kmapuni ya Rak Kaolinic Limited.
Kwa upande wa Wilaya ya Mkuranga Takukuru iliweza kufanikiwa
kuwarejeshea wakulima wa chama cha msingi cha Kimanzichana kusini kiasi
cha zaidi ya shilingi milioni 34 ambazo walikuwa wamedhulimiwa na
viongozi wa bodi ya Amcos na kampuni ya Cofee Traders.
No comments:
Post a Comment