Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika mkutano na wadau wa zao la korosho
kutoka wilaya mbali mbali za Mkoa huo kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali
kuhusiana na msimu mpya wa uuzaji wa korosho pamoja na kuzungumzia changamoto
mbali mbali zinazowakabili wakulima ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
NA VICTOR MASANGU, MKURANGA
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amepiga amekemea na kupiga marufuku
kwa baadhi ya wakulima kuuza zao la korosho kwa kutumia mfumo ambao
haukubaliki unaojulikana kama kang’omba na badala yake wahakikishe
wanazingatia mwongozo uliwekwa na serikali wa kuuza korosho hizo kwa kutumia
mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuepukana na changamoto za kuwanyonya na
kuwadhulumu haki zao wakulima.
Ndikilo
ametoa agizo hilo wakati wa mkutano na wadau mbali mbali wa zao la korosho
pamoja na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika pamoja na wakuu wa idara
mbali mbali kwa ajili ya kuweza kujadili namna ya kuweka mikakati ambayo
itaweza kuwasaidia wakulima kuuza korosho zao katika msimu unaokuja
ikiwemo kuzitatua changamoto zinazowakabili.
“Sisi kama serikali ya Mkoa wa Pwani lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunawasaidia wakulima wetu wa zao la korosho kwa kuweka mipango mizuri na mikakati ambayo itaweza kusaidia kabisa kuondokanana nah ii hali ya kuwanyonya wakulima kwa kutumia mfumo wa kangomba hii haikubaliki hata kidogo kikubwa hapa inabidi vyama vya msingi viweze kulisimamia ili kwa kutumia mfumo halali wa stakabadhi ghalani”alisema Ndkilo.
Pia
Ndikilo alisema kwamba katika kutimiza malengo amabyo wamejiwekea ni lazima
wakulima wote wa zao la kurosho kuhakikisha kwamba wanazingatia taratibu zote
za kilimo kwa kufanya usafi wa mashamba yao na kutoka uchafu wote ili korosho
zisiweze kuharibika na hatimaye kuweza kupata korosho nzuri yenye ubora ambao
unaweza kuwafanya wapate wanunuzi wengi.
Kadhalika
aliongeza kuwa kilimo cha zao la korosho ni mkombozi mkubwa kwa wananchi
kutokana na asilimia zaidi ya 80 wanategemea zao hilo katika kujiingizia kipato
chao na kuondokana na wimbi la umasikini hivyo ndio maana serikali imeamua
kulitilia mkazo suala hilo ili kuonyesha kwamba linaweza kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo na kukuza uchumi wan chi.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa waliwaasa viongozi wa vyama vya msingi vya
ushiriki kuwepo mipango madhubuti ya kuwatengenezea mazingira ambayo ni sahii
wakulima wa zao la korosho katika kuelekea msimu mpya wa uuzaji ili waondokana
na changamoto ya upatikanaji wa kupata soko kwa urahisi sambamba na kuzihifadhi
katika maghala ambayo yametengwa maalumu.
Nao
baadhi ya wakulima wa zao la korosho ambao wamehudhulia katika mkutano huo wa
wadau hawakusita kutoa kilio chao kwa Mkuu wa Mkoa kuhusiana na changamoto
inayowakabili ya ukosefu wa vifaa maalumu kwa ajili ya kupimia ubora wa
zao hilo pamoja na kuimba serikali iweze kuwasaidia kwa hali na mali
upatikanaji wa pembejeo za kilimo pamoja na magunia.
Naye
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Dolpine Magere amebainisha kwamba katika
msimu ulipita kulikuwepo n achangamoto mbali mbali ambazo ziliweza kujitokeza ikiwemo
kuwepo kwa mvua kubwa ambazo zilipelekea baadhi ya korosho kuharibika hivyo kwa
sasa wamejipanga katika kujiandaa na msimu mwingine ambao unakuja.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dolphine Magere akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na wakulima kuhusiana na mikakati na mipango ambayo imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wa zao la korosho ili kuweza kujiandaa na msimu mpya wa zao hilo.
Alisema zao la kurosho katika mkoa wa Pwani linachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato na kukuza uchumi kwa wananchi hivyo ni vema litakitiliwa mkazo mkubwa ili wakulima waweze kunufaika kupitia zao hilo ambapo aliwahimiza waweze kuzingatia taratibu zote wanazopatiwa na wataalamu ili korosho zao ziweze kuwa na ubora mzuri.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma amesema kwamba ili
kuweza kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wakulima ni lazima
kuwashirikisha mabwama shamba katika kila hatua mbao wataweza kutoe elimu zaidi
juu ya upandaji, ulimani pamoja na utunzaji wa zao hilo kwa kuzingatia
misingi ya taratibu zote zilizowekwa lengo ikiwa kupata ubora unaotakiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Shaibu Mnunduma akielezea jambo kuhusiana na jinsi alivyojipanga kikamilifu katika kuwasaidia wakulima wa zao la korosho kwa kusaidiana na maafisa wa kilimo pamoja na mabwana shamba ili kuwawezesha watimize malengo yao katika msimu mpya wa korosho.
Kilimo
cha zao la korosho katika Mkoa wa Pwani kimekuwa ni moja ya mkombozi mkubwa
katika kuwakomboa wananchi kuweza kuondokana na wimbi la umasikini na kuongeza
pato la Taifa hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka serikalini ili
kuweza kuondokana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wakulima hao.
No comments:
Post a Comment