Breaking News

Dec 21, 2020

WADAU WAPONGEZA IDARA YA AFYA MOROGORO,KIPINDI CHA COVID 19

 

        MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO,SHEILLA LUKUBA

Wadau wapongeza Idara ya afya Morogoro,kipindi cha COVID-19 

Na Lilian Lucas,Morogoro

Wakati Maambuki ya COVID-19 katika ukanda wa Afrika yameongezeka kwa kasi katika miezi miwili iliyopita, hali hiyo katika mkoa wa Morogoro wananchi wamekuwa wakiendelea na shughuli zao za kiuchumi katika mikusanyiko mbalimbali.

Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro akiwemo mzee fuko Kitenge amesema kuwa hali ya ugonjwa wa corona kwa Tanzania kasi yake imepungua kwa asilimia kubwa hali ambayo imesaidia wananchi kuondokana na hofu na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.

“Ninapongeza idara ya afya manispaa ya Morogoro na mashirika mbalimbali na wadau wa afya ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuwaelimisha wananchi kuzingatia kanuni za afya”Alisema Kitenge

 Aidha,mkurugenzi wa shirika la hope sport promotion,Bonface Ngonyani ni miongoni mwa wadau ambao walijitokeza katika manispaa ya Morogoro kipindi cha corona kupitia kila kata 19 zilizopo manispaa ya Morogoro katika kuwaelimisha umma juu ya kuzingatia misingi ya afya ili kuepuka maamuziki mapya dhidi ya covid 19.

Ngonyani alisema ya kuwa wakati wakiendesha elimu kwa wananchi kuzingatia kanuni za afya kwa kutumia maji tiririka walipewa ushirikiano mkubwa na idara ya afya ya Manispaa ya Morogoro ambapo walisimamia kikamilifu kwamba wananchi wanakuwa salama.

Alitaja njia walioitumia katika kufikisha ujumbe ni pamoja na kuandaa vipeperushi,kutumia vyombo vya habari ikiwemo vipindi vya redio ambapo walitumia redio Abood,magazeti na kwenye mikusanyiko ya watu na kugawa vitakasa mikono(sanitizer).

“tuligawa sabuni,ndoo za kunawia hasa kwenye mikusanyiko ikiwemo stendi na sokoni,tumefanikisha,tunaishukuru sana idara ya afya ya manispaa ya Morogoro imetupa ushirikiano mkubwa”alisema.

 Hali ya ugonjwa wa corona ikisisitiza hitaji la hatua za afya za umma zilizoimarishwa ili kuzuia kuongezeka kwa maambukizi, hasa wakati watu wanapokusanyika au kusafiri kwa sherehe za mwisho wa mwaka, imeeleza taarifa ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, iliyotolewa mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo.

No comments:

Post a Comment