BIL 298 KUTENGWA PWANI MIRADI
YA MAENDELEO,MISHAHARA
NA
VICTOR MASANGU ,PWANI
KIKAO
maalumu cha kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Pwani kimeazimia kwa pamoja kupitisha
kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 298 kwa kipindi cha mwaka wa
fedha 2021/2022 ambacho kimeombwa kwa ajili ya utekelezaji wa
majukumu yake mbalimbali ikiwemo mishahara ya watumishi pamoja na ujenzi wa
miradi ya maendeleo.
Hayo yamebainishwa na Mchumi wa Mkoa wa Pwani, Gerald Mbosoli
wakati akisoma taarifa ya mapendekezo wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha kwa
kipindi cha 2020 /2022 ambapo kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
serikali,viongozi wa dini ambao kwa pamoja waliweza kuiunga mkono bajeti hiyo
kwa asilimi 100 ambayo itakwenda kuleta chachu ya maendeleo.
Alibainishwa kwamba, kiasi hicho kilichoombwa kinaongezeka kwa
kiasi cha asilimia 9.38 ikilinganishwa na bajeti inayoendelea kutekelezwa na
kwamba maeneo ambayo yameongezeka ni katika matumizi mengineyo katika
sekretarieti ya Mkoa ikiwemo upande wa mishahara ya halmashauri pamoja na
mapato ya ndani.
Aidha, Mchumi huyo wa Mkoa, alisema kwamba, licha ya
bajeti hiyo kupitishwa kwa kishindo na wajumbe lakini kumekuwepo na
baadhi ya chanangamoto katika suala zima la mianya ya utoroshaji wa mapato
kutokana na uwepo wa bandari bubu pamoja na njia ambazo sizizo rasmi.
Pia, alisema kwamba, sababu ambazo zinapelekea kutofikia
malengo katika ukusanyaji kwa baadhi ya halmashauri ni kushindwa
kukusanya ushuru wa madini ya ujnenzi pamoja na baaadhi ya wananchi wengine
kutokuwa tayari kwa ajili ya kulipia kodi na ushuru wa hiari.
Kwa Upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo
amesema kwamba mpango wa bajeti hiyo pindi itakapotishwa Waziri mwenye
dhamana itakwenda kuleta mabadiliko chanya zaidi kwa wananchi katika
suala zima la kimaendeleo na kwamba ana matumaini makubwa ya
mapendekezo hayo ya bajeti yataweza kuwa ni mkombozi katika kuhudumia wananchi.
Mhandisi Ndikilo, ameziomba halmashauri zote tisa za Mkoa wa
Pwani kuhakikisha kwamba wanaweka mipango madhubiti ya kuweza kubuni vyanzo
vipya vya mapato ambavyo vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza
pato kuliko kutegemea chanzo kimoja katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.
“Kitu kikubwa ninachowaomba wakurugenzi wa halmashauri zote tisa
zilizopo Mkoa wa Pwani, ni lazima sasa tuweze kupambana zaidi katika ukusanyaji
wa mapato maana kuna baadhi ya halmashauri hapa bado hazijatimiza malengo ambayo
yamewekwa na serikali naona nyingi bado zipo chini ya asilimia 50 na chache tu
ndio zimeweza kuvuka juu ya asilimia 50.”alifafanua Ndikilo.
Dr. Delphine Magere ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kwa
upande wake, alisema kwamba katika kipindi cha mwaka wa 2021/2022 mkoa wa Pwani
utakuwa ni vipaumbele vipatavyo tisa ikiwemo kuhakikisha kwamba inasimamia hali
ya ulinzi na Usalama, kusimamia utekelezaji wa mkakati wa Taifa dhidi ya
mapambano dhidi ya rushwa.
Kadhalika aliipongeza serikali ya ya awamu ya tano kwa kuweza
kutatua baadhi ya chagamoto ikiwemo kutekeleza ujenzi wa bandari ya Nyamisati,
Kivuko cha kisasa cha Mv- Kilindoni, kutoa magari 11 kwa ajili ya wakuu wa
Wilaya pamoja na makatibu Tawala wa Wilaya ambayo yameweza kuwa mkombozi mkubwa
katika utekelezaji wa makukumu ya ya ya kuwatumikia wananchi.
Alivitaja vipaumbele vingine, kuwa ni kusimamia utekelezaji wa
shughuli za masuala ya mtambuka VVU, ukimwi , magonjwa yasiyo ya
kuambukiza, lishe pamoja na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo pamoja na kuimarisha
usimamizi na ufutatiliaji wa ukusanyaji wa mapato, pamoja na kuweza kubuni
vyanzo vipya vya mapato vya ndani katika halmashauri husika.
Kadhalika, alifafanua kwamba vipaumbele vingine, vitakuwa ni
uandaaji wa mazingira ya uwezeshaji kwa ajili ya uwekezaji na ujenzi wa viwanda
mbali mbali, pamoja na uboreshaji wa miundombinu katika sekta ya elimu
pamoja na afya, pamoja na kutilia mkazo zaidi katika sekta ya kilimo mifugo
pamoja na masuala ya uvuvi.
Katika hatua nyingine jambo lingine ni kuhakikisha wanasimamia
stahiki za watumishi ikiwemo pamoja na ulipaji wa madeni lengo ikiwa ni kuwapa
molali zaidi ya watumishi waweze kufanya kazi kwa weledi ambao unatakiwa kwa
kuzingatia msingi ya kazi iliyowekwa.
Nao baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika kikao hicho walitoa
pongezi kwa uongozi mzima wa Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuweka vipaumbele ambavyo
vitaweza kuwasaidia wananchi wanyonge na kwamba mapendekezo hayo ya mpango wa
bajeti yatasaidia kutatua changamoto zinazowakabili katika suala la huduma za
kijamii sambamba na kuwapatia watumishi stahiki zao.
No comments:
Post a Comment