KIWANDA CHA KUCHAKATA MIHOGO KUJENGWA CHALINZE
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarist Ndikilo akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la muhogo katika Mkoa wa Pwani ambacho kimeweza kuwajumuisha viongozi mbali mbali wa serikali, wakulima na taasisi binafsi kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa mstaafu Mwantumu Mahiza
NA
VICTOR MASANGU, PWANI
SERIKALI
Mkoani Pwani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa zao la Korosho
wameazimia kwa pamoja kujenga ujenzi wa kiwanda kikubwa kwa ajili ya kuchakata
zao la Muhugo ambacho kitajengwa katika eneo la Chailinze lililopo katika
halmashaurli ya Chalinze Wilayani Bagamoyo kwa lengo la kuwakomboa
wakulima wa zao hilo kuondokana na changamoto
zinazowakabili katika suala zima la upatikanaji wa soko. la uhakika
Maazimio
hayo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata zao la Muhogo, yamefanyika
katika mkutano wa wadau wa zao la muhogo katika Mkoa wa Pwani ambacho kimeweza
kuwajumuisha viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wadau wa zao hilo
wakiwemo wakulima kwa lengo la kuweka mikakati na kujadili
changamoto zinazowakabili wakulima hao wa zao la muhugo.
Akizungumza
katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarist Ndikilo ambaye
alikuwa ni mwenyekiti katika mkutano huo, alisema
kwamba lengo kubwa serikali ni kuweka mikakati madhubuti
ambayo itawasaidia kuwakomboa wakulima wa zao la muhogo hivyo ujenzi
wa kiwanda hicho utakuwa ni mkombozi mkubwa na chachu ya kuleta
mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Alisema kuwa zao la Muhogo ni moja ya zao muhimu na kwamba
likitumika vizuri linaweza kuwaongezea wakulima kipato,pato la Mkoa na hata
kujenga uchumi wa Taifa.
Ndikilo alisema kuwa, wakulima wengi wanalima zao hilo huku
wakiwa hawana utaalamu wala elimu ya kutosha juu ya zao hilo wakati maafisa
ugani wapo hivyo ni muda muafaka kwa maafisa ugani kuona namna ya kuwatembelea
wakulima kwa kuwapa elimu ya zao hilo.
Alisema kuwa mkoa wa Pwani una jumla ya hekta 3,353,900 ambapo
eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 1,933,224 sawa na asilimia 57.66 ya eneo
lote.
Alisema, pamoja na kuwepo kwa ukubwa wa eneo hilo lakini bado
Muhogo hulimwa kwa kiasi kidogo ikiwa ni wastani wa hekta 60,703 na kuzalisha
tani 500,000 hadi 650,000 kwa mwaka sawa na asilimia asilimia tatu ya eneo hilo.
" Kwa upande wa tija nayo ipo chini kwa miaka mitano
iliyopita uzalishaji kwa eneo ni wastani wa tani 6.5 hadi 7.6 kwa hekta
ingawa yapo maeneo machache hasa Kibiti na Rufiji ambako tija ni kati ya tani 9
hadi 18 kwa hekta wakati tija inayopendekezwa kitaalamu kuwa ni tani 20 kwa hekta"
alisema Ndikilo.
Kuhusu usindikaji mkuu huyo wa mkoa, alisema mkoa bado
haufanyi vizuri pamoja na kuwepo kwa juhudi za kuanzisha vikundi na Viwanda vya
usindikaji kwani vikundi 32 vilivyopo katika Mkoa huo havisindiki mihogo kwa
madai ya kukosa soko la uhakika.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wadau wa zao la Muhogo (TACAPPA)
Mwantumu Mahiza, alisema endapo wakulima watahamasishwa kuhusiana na zao hilo
litawasaidia kujikwamua kutoka kwenye umasikini.
Mahiza, alisema maaofisa ugani wanatakiwa kusaidia kutoa elimu
kwa wakulima ili waweze kulima zao hilo kitaalamu na kupata mbegu bora na
kwamba bila hivyo hakuna mafanikio yatakayopatika.
Alisema,chama hicho kimejipanga kupambana na vikwazo vya soko la
zao hilo ambapo vikitolewa wakulima watachangia kuinua uchumi wa taifa na
kuondoa umasikini wa kaya.
Mahiza alisema kuwa, kwa sasa Taccapa kipo katika mpango wa
kujenga kiwanda kikubwa cha Muhogo ambacho kitahudumia Mikoa ya Kanda ya
Mashariki na Kati na kufanya Muhogo kupata soko kubwa zaidi.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dkt.Dolphine
Magere,alisema kuwa kikao hicho kinalenga kutoa dira ya kuhakikisha zao Muhogo
linapata hadhi kama mazao mengine.
Magere alisema kuwa baada ya kikao hicho timu mbalimbali kupitia
Halmashauri zitaundwa kwa kuwashirikisha maafisa ugani ili kusudi wawe karibu
na wakulima wa zao hilo.
Mmoja wa wakulima aliyeshiriki kikao hicho Gosbert Joshua
aliomba kuwepo na kituo cha kuzalisha mbegu za Muhogo kuondoa usumbufu wa
kuzifuata mbali na wanapoishi.
No comments:
Post a Comment