MA-DC PWANI WASHAURIWA KUFUATILIA LISHE KWA WANANCHI WAO
NA VICTOR MASANGU
WAKUU wa Wilaya mkoa wa Pwani wameshauriwa kuhakikisha wanasimamia kwa karibu katika
kutatua changamoto zilizopo katika baadhi ya maeneo yanayokabiliwa na uwepo
kwa lishe duni kwa wananchi na udumavu, hali inaweza kukwamisha shughuli za kuleta maendeleo.
Kauli hiyo
ameitoa wakati wa kikao maalumu cha kufanya tathimini ya tatu mkataba wa
mambo yanayohusiana na lishe ngazi ya Mkoa ambapo kimehudhuriwa na
viongozi mbali mbali wa serikali, wadau wa maendeleo, waganga wakuu wa Wilaya,
wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa Wilaya sambamba na wakurugenzi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere amewahimza viongozi mbalimbali
wa Wilaya ambazo hazijafanya vizuri kujitahidi zaidi katika kukabiliana na
lishe duni hasa kwa wananchi wote wa waeneo yao ili kuondokana na
changamoto hizo ambayo ipo katika baadhi ya Wilaya.
“Kwa kweli
suala la mambo ya lishe katika Mkoa wetu wa Pwani ni jambo ambalo lipo
nyeti sana kwa hivyo ninawaomba viongozi wote katika ili tuweze kushirikiana
kwa pamoja kwa lengo wa kuwahimiza wananchi juu ya umuhimu mkubwa katika mambo
ya lishe na manufaa yake ,”alisema Dk, Mgere.
Dk. Magrere
alifafanua kuwa ana imani kubwa endapo viongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na
wananchi wao wanaweza kuweka mipango madhubuti pamoja na kuwa bega kwa bega na
watalaamu wanaweza kusaidia kuleta mabadiliko katika masuala ya Lishe.
“Napenda
kuchukua fursa hii ya kuwakumbusha viongozi wa baadhi ya Wilaya ambazo kwa
namna moja au nyingine sehemu zao ambazo wanazifanyia kazi hazijafanya vizuri
sana katika suala la lishe ambalo leo tumeakua kukutana kwa pamoja na viongozi
wa halmashauri zote tisa za Mkoa ili kuweza kuona namna ya kulijadili na
kulitafutia ufumbuzi,”aliongeza Dk. Magere.
Nao baaadhi
ya viongozi na wadau ambao wameshiriki katika kikao hicho wameahidi
kuyafanyiakazi maagizo yote ambayo yametolewa na kwamba wataweka mipango
madhubuti ambayo katika siku za usoni itaweza kubadilisha kabisa changamoto
ambazo zinawakabili katika mambo ya masuala ya lishe ili wananchi wasiwe
wadumavu.
Kikao hicho
kimefanyika kwa lengo la kuweza kujadili mikakati ya kusaidia mambo mbali mbali
yanayohusiana na lishe ikiwemo kujadili changamoto zilizopo katika halmashauri
zote tisa za Mkoa wa Pwani ili kuweza kuzitafutua ufumbuzi wa kudumu.
No comments:
Post a Comment