WALIMU KISARAWE WATAKIWA KUWAJIBIKA,KUACHA UZEMBE
NA
VICTOR MASANGU, KISARAWE
WALIMU wa
shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani
Pwani wametakiwa kuachana na tabia ya uzembe na badala yake wahakikishe
wanatekeleza majukumu yao kwa nidhamu na weledi kwa lengo la kutoa
elimu bora ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wanafunzi katika
kuongeza kiwango cha ufaulu na kufanya vizuri katika masomo yao.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,
Mussa Gama wakati wa hafla fupi ambayo iliandaliwa maalumu kwa ajili ya kuwapongeza
walimu na baadhi ya shule vizuri katika mitihani ya Taifa na kuhudhuliwa na
viongozi mbali mbali wa serikali, madiwani, wakuu wa idara pamoja na walimu
kutoka shule mbali mbali.
Gama alisema
kwamba wigo wa elimu ni mpana sana hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kutoka
kwa walimu wenyewe pamoja na wanafunzi katika suala zima la kuwa na nidhamu
pamoja na maadili na kuwaasa wanafunzi kuzingatia maelekezo na mafundisho mbali
mbali ambayo wanapatiwa na wazazi na walezi pindi wanapokuwa nyumbani pamoja na
mashuleni.
“Wazazi na
walezi ni jukumu lenu kwa kushirikiana na walimu kuhakikisha kwamba mnasimamia
nidhamu ya watoto wenu na kuhakikisha kwamba vijana wao wanafika shuleni bila
kutegea na kwamba wanasoma kwa bidii hivyo katika hili ninawaomba sana mkalisimamie
ili siku za usoni liweze kuleta matokeo chanya ya kuongeza kasi ya kufanya
vizuri,”alifafanua Gama.
Kwa
Upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe Mwanana Msumi aliwataka walimu
kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia misingi ya nidhamu
kwa lengo la kuweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kuboresha sekta ya
elimu katika shule mbali mbali zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe.
“Kwa kweli
kwa upande wangu napenda kuchukua fursa hii kuwaaagiza walimu wote kuhakikisha
wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na tena kwa weledi wa hali ya juu nia yetu
ni kujenga misingi mizuri ya kuboresha sekta ya elimu katika shule zeto mbali
mbali zilizopo katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na kwamba kitu kikubwa
ni kuweka nidhamu ili kutimiza malengo waliyojiwekea,”alisema Mwanana.
Aidha Katibu
Tawala huyo alisema kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha kwamba inawawekea
mazingira rafiki kwa wanafunzi pamoja na walimu ili kuweza kuleta mabadiliko
chanya katika kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu sambamba na kuhakikisha
wanaboresha miundombinu ya madarasa ili wanafunzi wasiweze kusoma katikahali ya
mlundikano.
Kwa Upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe
aliwahimiza wazazi na walezi kuweka misingi imara ya kuhakikisha wanasimamia
kwa umakini suala la mwenendo wa watoto wao katika uwajibikaji wa kwenda
shule pamoja na kuwahimiza wajitahidi kwa hali na mali waweze kusoma kwa bidii.
Naye
Diwani wa Kat ya Manerumango Hamisi Dipakutile alifafanua kwamba ili kutimiza
azama y serikali katika kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi inapaswa
zifanyike juhudi za makusudi kwa walimu kuhakikisha wanaachana na tabia ya
uzembe na badala yake waongeze bidii ya kufuwafundisha wanafunzi bila kutegea
kwani baadhi yao wamekuwa ni wazembe.
“Ili jambo
la elimu inapaswa kwa kweli litiliwe mkazo mno maana kuna baadhi ya shule kwa
kipindi hiki cha mwaka wa 2012 hadi leo hii mwezi wan ne wamesoma topiki moja
tu, nah ii inatokana na baadhi ya walimu wetu kutotekeleza majukumu yao
ipasavyo kwa hivyo mimi naomba jambo hili liweze kufanyika kazi ili elimu yetu
iweze kufika mbali zaidi na kufanya vizuri katika masomo yao,”alisema
Dipakutile.
Abel Mudo ni
Diwani wa kata ya Kisarawe naye alibainisha kuwa kumekuwepo na tabia ya wakuu
wa shule kutotimiza wajibu wao ipasavyo na kupelekea hata walimu wengine
kushindwa kufundisha kama inavyotakiwa hivyo ameahidi kulivalia njuga suala
hilo kwa nia ya kuleta chachu ya elimu katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
katika sekta ya elimu kwa shule za msingi na sekondari.
No comments:
Post a Comment