WATUHUMIWA 23 MBARONI PWANI, WADAIWA KUIBA MSIBANI
NA VICTOR MASANGU,PWANI
JESHI la
polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa
23 ambao wamejihusisha katika makosa mbali mbali likiwemo la kufanya
uharifu wa wizi wa kuiba vitu mbalimbali katika msiba mmoja
ulitokea mlandizi Wilayani Kibaha, pamoja na wengine kukutwa na
madawa ya kulevy aina ya bangi, wizi wa laini 74 za simu ambazo zilikuwa
zikitumika katika kufanyia utapeli.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Wankyo Nyigesa
akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, amebainisha kwamba
matukio hayo yametokea kwa nyakati tofauti na kwamba wezi hao walikwenda katika
msiba huo na kukuta watu wamelala ndipo walivunja mlango na kisha kuingia ndani
na kuwapulizia watu dawa.
Wankyo, alisema tukio hilo la
wizi uliofanyika msibani baada ya mazishi watu wakiwa wamelala ndani wezi
walivunja mlango wa nyumba wafiwa wakiwa wamepuliziwa dawa ndipo wezi wakaiba
vitu mbali ikiwemo Televisheni tatu, Mbili aina ya Startimes inch 32 na
moja aina ya UK inch 21,Simu za mkononi tano. (Tecno 3, Itel 01, Bontel
1)
Alivitaja vitu vingine vilivyoibiwa msibani kuwa ni pamoja na
Radio mbili aina ya Sonny Spika nne, Deki mbili. Moja aina ya LS na nyingine
aina ya HITACH,King’amuzi kimoja aina ya Startimes.
Kamanda Wankyo amesema Jeshi hilo limefanya operesheni kwa
kipindi cha wiki moja kuanzia tarehe 01/03/2021 hadi tarehe 10/03/2021 katika
Wilaya zote tano za Polisi ambapo Watuhumiwa wengi Kati ya hao 23
walikamatwa huko mlandizi wilayani kibaha.
"Madhumuni ya misako hiyo ilikuwa ni kudhibiti na kuzuia
matukio ya makosa ya wizi, Uvunjaji na matumizi ya madawa ya
kulevya" alisema Wankyo.
Katika operesheni hii tumefanikiwa kukamata Watuhumiwa hao
walikamatwa na vitu vingine mbalimbali kama Bhangi kilo 296, Miche ya
bhangi iliyokutwa imelimwa nyumbani kwa mtuhumiwa katikati ya shamba la
mahindi àmbapo mtuhumiwa alikuwa akitunza kwa kupalilia bhangi hizo sawa zao
lake la mahindi na pia alikuwa na Mirungi bunda 35 huko wilayani Bagamoyo.
"Laini 74. Kati ya hizo laini 56 ni mpya na laini 18
zinazotumika kufanya utapeli zikiwa zimesajiliwa kwa jina moja la Mosses
Cosmas" alisema Wankyo.
Aidha Scanner moja aina ya Mantra kwa ajili ya kuchukua alama za
vidole (Finger print) Mashine ya kusajilia laini Solar power, Makoti 12 ya
Kampuni ya ulinzi ya SGA, Pikipiki moja aina ya SAN LG nyekundu yenye namba za
usajili T.659 CCA Ikiwa ni pamoja na Pombe ya gongo lita 49.
Hata hivyo, Kamanda Wankyo, amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa
Pwani linawahakikishia wananchi kuwa linaendelea kuimarisha ulinzi na usalama wakati
wote na operesheni hizi ni endelevu.
Alisema Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani baada ya
uchunguzi kukamilika."Wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la
Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wachukuliwe hatua za
kisheria na kuufanya Mkoa wa Pwani kuendelea kuwa shwari" alisema Wankyo.
No comments:
Post a Comment