SAYARI MODERN TAARAB: YAJA NA KIBAO SENSA NDIYO HABARI YA MJINI TANZANIA
Na Thadei Hafigwa,Morogoro
KIKUNDI cha muziki wa
Taarabu,Sayari Modern Taarab kilichopo Manispaa ya Morogoro kimetoa kibao
kipya cha kuhamasisha zoezi la
kuhesabiwa watu hapa nchini(sensa) linalotarajiwa kufanyika Agosti 23,mwaka huu
ikiwa ni moja ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita.
Msemaji wa Sayari Modern
Taarab,Bi.Mariam Mambo akiongoza na wasanii wenzake,Zainabu Saleh na Sharifa
Issa amesema kundi lao lilianza mwaka 2019 wakitumbuiza maeneo mbalimbali mjini morogoro baada ya
kuivishwa na mwalimu wao Ramadhan Kisoro,mwalimu na mwimbaji wa kujitegemea
kutoka Jijini Dar es Salaam.
Mambo alisema kuwa mwanzoni
kabla hawajapata uzoefu wa utunzi wa nyimbo walikuwa wakinukuu tungo mbalimbali
zilizowahi kutungwa na kuchezwa na wasanii mbalimbali wenye uzoefu na nyimbo za
taarabu.
Aidha,Mambo amesema kuwa
kabla ya kujiuhusisha na muziki wa taarabu walikuwa wakishiriki kwenye sanaa ya
maonesho kwa kuendesha kampeni mbalimbali utuatiliaji wa rasilimali za umma
kupitia sanaa shirikishi jamii pamoja na miradi ya kupinga ukatili wa kijinsia
kupitia asasi za kiraia.
Alisema kikundi chao cha
Sayari Modern Taarab baada ya kuona serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kuzindua kampeni za
uhamasishaji juu ya watanzania kuhesabiwa(Sensa) wameguswa na jambo hilo hivyo
wakaona watoe mchango wao.
Mambo alisema kuwa kuna
dhana iliyopo kwenye jamii kwamba ukihesabiwa unapuza umri wa kuishi,au ni
kujitabilia kifo,kwamba dhana hiyo ni potofu kwani hakuna uhusiano wowote kati
ya suala la kuhesabiwa na umri wa mtu wa kuishi.
“Sisi kikundi cha sayari
Modern Taarab tumejidhatiti kuunga mkono juhudi za serikali katika kufanikisha malengo
ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanahamasika kuhesabiwa.”Alisema.
KIKOSI CHA WASANII WA SAYARI MODERN TAARAB CHA MJINI MOROGORO WAKIWA KATIKA KASHKASHI ZAO,SENSA NDIYO HABARI YA MJINI KAHESABIWE.
Alisema kuwa hadi sasa Sayari
Modern Taarab toka watoe kibo hicho kipya cha kuhamasa juu ya sensa vituo vya
redio na luninga vilivopo ndani ya mkoa wa Morogoro na nje ya Morogoro
wanarusha na kucheza mara kwa mara.
Kwa upande wake Zainab
Saleh,msanii wa kikundi hicho alisema wapo tayari kushirikiana na wadau wengine
katika kuhamasisha masuala mbalimbali ya kijamii kupitia sanaa shirikishi
ambayo kurahisisha uwasilishaji wa ujumbe kwa jamii.
Zainab amesema ni muda
muafaka kwa jamii kutambua mchango wa wasanii kwa kuwa ulimwengu wa sasa sanaa
imekuwa ni sehemu ya ajira,hivyo iwapo vijana wakapewa moyo na hamasa kutaleta
matokeo chanja katika maendeleo ya watu.
Msanii mwingine wa kikundi
cha Sayari Modern Taarab,Sharifa Idd alisema
kuwa dhana ya waimbaji wa muziki wa taarab ni wahuni si sahihi na badala yake
watambue ya kuwa wapo wasanii wa muziki wa taarab wametoa mchango mkubwa hapa
nchini na nje ya nchi.
Sharifa amemtaja miongoni
mwa wasanii hayo ni Bi Kidude alikuwa ni mwimbaji wa muziki wa taarab alikuwa
ni maarufu wakati wa uhai wake na hata baada ya kufa,ambapo watu wamekuwa
wakimkumbuka na kumuezi kutokana na kazi alizofanya ndani ya taifa la Tanzania na
pia ikiwemo Afrika mashariki,ulaya na Asia.
No comments:
Post a Comment