Breaking News

Jul 28, 2022

WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KWENYE SENSA

 Aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Martine Shigela (sasa mkuu wa Mkoa wa Geita)akimlisha kipande cha keki Mzee Stephen Mashishanga,Mkuu wa Mkoa mstaafu ikiwa ni ishara ya kumtakia heri kwa siku ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 88,hafla hiyo imefanyika nyumbani kwake mjini Morogoro.


      WATANZANIA WAHAMASISHWA KUSHIRIKI KWENYE SENSA

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

WATANZANIA wametakiwa kushiriki kwenye sensa ya watu na makazi ili kuunga mkono malengo ya serikali kwamba ifikapo Agosti 23,2022 watanzania katika makundi yote,wazee,wake kwa waume,watoto na watu wenye ulemavu wapate kuhesabiwa.

Wito huo umetolewa na ,Dk.mchungaji Emanuel Falanta katika hafla maalum ya kumtakia heri Mkuu wa mkoa mstaafu Stephen Mashishanga katika siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika Julai 27,mjini Morogoro.

Katika Hafla hiyo ilihudhuria na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro,Dorith Mwamsiku,Martine Shigela aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyehamishiwa Mkoa wa Geita na viongozi wa dini.

Mchungaji Faranta ambaye pia ni mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dodoma,katika ibada hiyo maalum alisema kuwa sensa umuhimu wa sensa ni agenda mtambuka kwa sasa kwa sababu itarahisisha serikali kuwa na takwimu sahihi idadi ya watu,umri,jinsi zao,elimu na nafasi zao kwenye jamii katika kuweka mipango ya maendeleo kwa wananchi.

“Ninatoa wito kwa watanzania wote kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la kuhesabiwa kila kuacha mtu kwamba ifikapo Agosti 23,2022 tutoe ushirikiano kwa maafisa wa sensa wanapotufikia kwenye maeneo yetu.”Alisema Mchungaji Faranta.

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa mstaafu,Stephen Mashishanga alishukuru Mungu kwa kumpa afya njema kufikisha umri wa miaka 88 toka kuzaliwa kwake,kwa kuwa bila Baraka zake Mungu asingeweza kufanikisha jambo lolote.

Mzee Mashishanga pia alitoa wito kwa watanzania kumpa ushirikiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ili aweze kutokeleza majukumu yake bila kukwazwa na yeyote.

Alisema kuwa Rais Samia na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi taifa amekuwa akifanyakazi ya kuwahudumia watanzania bila ya kujali hali ya mtu,maeneo au ukabila hivyo anapaswa kuungwa mkono bila ya kumkwaza katika utendaji wake wa kazi.

Awali aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Martine Shigela ambaye katika uteuzi mpya amehamishiwa Mkoa wa Geita alimpongeza Mzee Mashishanga kwamba pamoja na kustafu kwake katika utumishi wa umma wakati wote amekuwa alitoa ushirikiano mkubwa ndani ya serikali na chama cha mapinduzi(CCM). 

Shigela alimweleza Mzee Mashishanga amekuwa na upendo mkubwa kwa wananchi wa Morogoro ambapo amekuwa akishiriki na kujitokeza katika shughuli mbalimbali za kijamii.

No comments:

Post a Comment