Na.Thadei
Hafigwa,Morogoro
JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro na Waandishi wa habari
wameazimia kutekeleza mambo manne katika utendaji wa kazi wao wa kazi ikiwa ni
hatua ya kimkakati katika kuendeleza mahusiano na mawasiliano ya kikazi ikiwemo
upatikaji wa taarifa kwa wakati na kukutana mara kwa mara katika taasisi zao.
Maazimio hayo yamefikia mjini Morogoro, katika mdahalo na kikao
kazi kati ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari ikiwa ni mwendelezo wa
mahusiano ya kikazi na ulinzi na usalama wa mwandishi wa habari,shughuli
iliyoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa
Habari(MOROPC) ,UTPC chini ya ufadhili wa shirika la IMS,akiwa ni mshirika mkuu
wa programu hiyo..
Akiongea kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,SP.
Morgan Marunda alitaja maazimo hayo ni Polisi Mkoa wa Morogoro na Waandishi wa
habari wameazimia kuendelea kuwa na mahusiano na mawasiliano ya kikazi.
SP. Morgan akianisha azimio lingine ni kwamba, vituo vya redio
na Luninga vilivyopo Mkoa wa Morogoro vitaendelea kutoa nafasi bure kwa jeshi
la polisi katika vipindi vya kuelimisha umma ikiwa ni mapango maalum
wa kuelimisha wananchi masuala mbalimbali katika upatikanaji wa huduma
zizotolewazo na Polisi ili kuleta ustawi wa taifa.
Kadhalika ,SP.Morgan alisema Jeshi la Polisi litatoa taarifa kwa
wakati kwa kufuata njia sahihi ili waandishi wa habari waweze kuhabarisha umma
katika masuala mbalimbali yanayotokana na kazi zinazofanywa na jeshi la Polisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Morogoro Press Club,Nickson
Mkilanya amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuonesha utayari wake wa kuondoa manung’uniko yaliokuwa yakiwasibu
waandishi wa habari mkoani hapa katika upatikanaji wa taarifa kwa wakati katika
Jeshi la Polisi..
Mkilanya amewashi waandishi wa habari kuendelea kuheshimu na
kufuata sheria wakati wanapotimia wajukumu yao ambapo pamoja na mambo mengine
waandishi wanapaswa kuunga mkono kampeni mbalimbali zinazofanywa na serikali
ikiwemo chanjo na sensa ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika Agosti
23,mwaka huu.
Aidha,katika tukio lingine Uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari
Mkoa wa Morogoro walitumia fursa hiyo kuendesha zoezi la uwagawaji wa
vizibao(press jacket) ili kumrahisishia mwandishi wa habari kutambuliwa kwa
urahisi wakati wa kutimiza majukumu yake kwa kuzingatia ulinzi na usalama
katika mazingira hatarishi.
Katika Mdahalo huo uliwashirikisha waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi,ambapo mada mbalimbali zilizotolewa ikiwemo mfumo wa utendaji wa jeshi la polisi katika utoaji wa taarifa kwa kuzingatia masilahi mapana ya wananchi,ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari yalioenda sambamba na kufikiwa kwa maazimio ya kikazi baina ya pande zote mbili(Jeshi la Polisi na Waandishi wa habari)
No comments:
Post a Comment