Na Thadei Hafigwa,Morogoro
KUTOKANA na mabadiliko ya
tabianchi uliosababisha kukosekana kwa upatikanaji wa maji ya kutosha katika
kipindi cha mwaka 2020 na 2021 umeathiri mradi wa upandaji wa miti katika shule
za msingi Luhundo na Bigwa,Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Shirika la
The society for Women and Aids in Afrika(SWAA),Helen Mbezi amebainisha hayo
mbele ya kamati ya mazingira ya baraza la madiwani, Manispaa ya Morogoro kwenye
ziara ya kutembelea maendeleo na changamoto zilizopo katika mradi huo.
Helen alisema kuwa katika
kipindi cha mwaka jana wameweza waliweza kuotesha kitalu cha miti 14,000 aina
ya graveria ambapo miti 7000 ilioteshwa katika shule ya msingi Luhundo na miti
7000 mingine ilioteshwa katika shule ya msingi Bigwa zilizopo halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro lakini miti hiyo kutokana na kuwepo kwa ukame
uliosababisha kunyauka kwa kukosa maji.
Mwenyekiti wa kamati ya
mazingira,Manispaa ya Morogoro,Hamis Kilongo pamoja na kulipongeza shirika la
SWAA katika harakati zake za utoaji wa elimu ya uhifadhi mazingira kwa wadau wa
mazingira wakiwemo madiwani,wananchi na wanafunzi,lakini amehidi kuhakikisha ya
kuwa miradi ya mazingira inapewa kipaumbele katika maeneo mbalimbali ya
manispaa ya Morogoro.
BAADHI YA WANANCHI WA KATA YA LUHUNGO WAKISIA MBEGU KWENYE VIRIBA TAYARI KWA KUOTESHA MITI YA MBAO NA MATUNDA INAYOTEKELEZWA NA SHIRIKA LA SWAA,LILILOPO MOROGORO
Kilongo amemhakikishia
Mkurugenzi wa shirika la SWAA kuwa changamoto ya ukosefu wa maji wataifanyia
kazi kwa kuwasilisha hoja hiyo katika vikao vya madiwani ili kupatiwa ufumbuki
ikiwemo kuwasiliana na wadau wengine wakiwemo MORUWASA kwa lengo la kutafuta
suluhisho la kudumu katika maeneo yanayotekelezwa mradi.
Aidha,Afisa elimu wa shule
za msingi,Manispaa ya Morogoro,Mwamsiku Masegenya ameahidi kushirikiana na
shirika la SWAA ili mradi wa upandaji wa miti uwe endelevu na kuwafikia
wananchi wengi ambapo alishauri kitalu vya miti vioteshe katika shule nyingine
za manispaa ya Morogoro ikiwemo shule ya msingi mzinga.
Mwamsiku pia amewapongeza
walimu wa shule za msingi zilizonufaika na mradi wa uhifadhi wa mazingira
waendelee kuotesha miti kwa kuhamasisha wanafunzi iwaweze kuwa na mwamko wa
kutunza mazingira wakiwa shuleni na nyumbani kwa manufaa ya sasa na vizazi
vijavyo.
No comments:
Post a Comment