Breaking News

Jul 20, 2022

SERIKALI YAJA NA MKAKATI WA KUBORESHA ZAO LA MKONGE

 


SERIKALI YAJA NA MKAKATI WA KUBORESHA ZAO LA MKONGE

Na Thadei Hafigwa,Morogoro

SERIKALI ya awamu ya sita imekuja na mkakati kabambe wa kufufua zao la Mkonge kwa kuunda kamati maalum ya kuratibu na kufanikisha kilimo cha zao la mkonge kwa wananchi wa mikoa ya Morogoro na Tanga ili kukidhi matakwa ya soko la ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amebainisha hayo mjini Morogoro na kuitangaza kamati hiyo kuwa itaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Adamu Malima kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Martine Shigela na kupewa hadidu rejea za kimkakati ikiwemo ugawaji wa mashamba ya mkonge kwa wananchi wadogo wadogo wa mikoa inayozalisha zao hilo.

Bashe amesema kuwa kamati hiyo ina wajumbe 11 itakamilisha kazi yao kwa muda wa mwezi mmoja ambapo itawajumuisha wajumbe kutoka taasisi za utafiti wa mbegu,wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na wadau kutoka sekta binafsi.

Alisema kuwa ili kufanisha lengo la kuendeleza zao la Mkonge serikali imeahidi kuwasiliana na wadau wa mazingira ili kuhakikisha ya kuwa kamba na vifungashio vya mazao ya kurosho kutumia malighafi ya zao la mkonge ili kuliongezea thamani na tija wa zao hilo hapa nchini.

Kadhalika, alisema wizara ya kilimo ipo katika hatua ya mazungumzo na ofisi ya makamu wa Rais Muungano na mazingira kuangalia namna ya kutunga kanuni itakayozuia mazao yote ya kilimo kutotumia malighafi na nyuzi zitokanao na plastiki badala yake vifungashio zitumike nyuzi za mkonge.

“Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha zao la mkonge linapata thamani ambapo fedha imetenga ajili ya ujenzi wa maabara ya utafiti wa mbegu za mkonge katika kituo cha utafiti cha TARI Mlingano cha mkoani Tanga” Alisema.

                                 ZAO LA MKONGE

Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akiongea kwa niaba ya kamati hiyo,amempongeza waziri wa Kilimo,Hussein Bashe kwa juhudi zake za kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza sekta ya Kilimo ikiwemo zao la Mkonge.

Shigela pia amemshukuru Waziri Bashe kwa kuonesha imani kwake kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya maalum ya kufufua zao la mkongena kwamba atahakikisha kuwa atatekeleza hadidu zote zilizoanishwa na wizara katika ufufuaji wa zao hilo la mkonge ambalo ni rafiki wa mazingira.

Saddy Kambona,Kaimu Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Mkonge,alisema hatua ya Waziri Bashe kuundwa kwa kamati hiyo ndogo kutaleta tija kubwa kwenye uzarishaji wa zao la mkonge kwani wakulima wadogo wana mchango mkubwa katika kuliendeleza zao la mkonge kwa kipindi kirefu.

Kambona alisema kuwa Bodi ya mkonge unatambua vema mchango wa wakulima wadogowadogo hivyo hatua ya serikali ya kufufua zao hilo litachangia kuboresha kipato chao na pato la taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa Uzarishaji na usambaji wa mbegu za mkonge kwa wakulima wadogo utaleta tija kwa kuwa serikali imetoa fedha kwa ajili kuendeleza zao hilo ili kuwafikia wakulima wa maeneo mengine yanayostawisha zao la mkonge. 

No comments:

Post a Comment