Breaking News

Jul 18, 2022

KENNETH WESTON SIMBAYA AMETANGAZWA RASMI KUWA BOSI MPYA UTPC

                                            BWANA KENNETH WESTON SIMBAYA

KENNETH WESTON SIMBAYA AMETANGAZWA RASMI KUWA BOSI MPYA UTPC

Na Lilian Lucas

Mkutano wa mashauriano kati ya UTPC na SIDA umeanza uliofanyika hivi karibuni Jijini Dodoma umetoa mwelekeo wa utekelezaji wa mpango mkakati wa miaka mitatu wa uendeshaji wa shughuli za Klabu za waandishi wa habari hapa nchini unasimamiwa na kuratibiwa na UTPC.

Katika Mkutano huo, uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa klabu wamehudhuria wakiwemo wawakilishi kutoka Sida.umefunguliwa rasmi na Rais wa UTPC Bw. Deogratius Nsokolo ambapo katika hotuba yake ya ufunguzi, ametangaza rasmi kupatikana kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa UTPC ambaye ni Bw. Kenneth Simbaya.

Pamoja na mambo mengine, Nsokolo ameishukuru Sida kwa kuendelea kuisaidia tasnia ya habari nchini kupitia UTPC kwani Sida wameridhia na kukubali kuendelea kufadhili tena UTPC kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Nsokolo ameongeza kuwa, katika kipindi hiki ambacho UTPC inapita kwenye mabadiliko makubwa ya uongozi,  inahitaji ushirikiano mkubwa baina ya viongozi wa UTPC na wanachama wake.

Aidha, alimshukuru sana Mkurugenzi anayemaliza muda wake Abubakar Karsan kwa weledi na umahiri kuitumikia UTPC na wanachama wake kwa uadilifu na ubunifu mkubwa.

Nsokolo amemhakikishia Mkurugenzi mpya wa UTPC  Kenneth Simbaya na kuahidi kumpa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha malengo yote yaliyopangwa..

Kwa upande wake Mkurugenzi mstaafu wa UTPC,Bw.Abubakar Karsan amesema huyo tayari kutoa ushirikiano kwa Mkurugenzi mpya pale atakapohitajika, na kwamba ataendelea kuwepo ofisini mpaka mwezi Desemba 2022 atakapostaafu rasmi.

No comments:

Post a Comment