RC ADAM MALIMA:HATUTAKI KWENYE MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI KULETEWA WANYAMA WALIOKONDEANA TUNATAKA WALIONONA
Na.Lilian Lucas,Morogoro
WASHIRIKI wa maonyesho ya wakulima NanenaneKanda ya Mashariki wametakiwa kuhakikisha wanapeleka bidhaa zenye ubora, kuelimisha, yakiwemo Mazao na Wanyama walionona na sio waliokondeana.
Mkuu Mkoa wa Tanga Adam
Malima, alisema hayo mkoani Morogoro kwenye kikao cha maandalizi ya Nanenane
kanda ya Mashariki, inayoundwa na Mikoa minne ya Dar es salaam, Pwani, Tanga na
wenyeji Morogoro ambapo maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika mkoani Morogoro
katika viwanja vya Julius Nyerere Agosti 1,2022.
Malima alisema kumekuwa na
tabia ya baadhi ya washiriki kwa maana ya watoa huduma kuleta bidhaa ambazo
hazina ubora na kufanya maonyesho kutokuwa na mvuto na kwamba sasa seriksli
itakagua kwa umakini wale wote watakaoleta bidhaa zao kwenye maonyesho hayo.
“Wanaoleta wanyama kwenye
Zoo walete Simba na wanyama wengine walionona, kuna wakati aliletwa Simba
kakondeanaa unajisikia aibu kumwangalia hii kwa sasa hatuitaki kwenye kanda
yetu,”alisema Malima.
Aidha alisema Maandalizi
yote yamekamilika, mashirika, taasisi za serikali na binafsi yanatarajiwa
kushiriki ni zaidi ya 500, katika maonyesho hayo watoto wadogo wataruhusiwa
kuingia bure huku wazazi ama walezi walioambatana nao wakilipia kiingilio cha
shilingi 1,000 kwa mtu mmoja.
Mkuu wa Idara ya Kilimo wa
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Michael Waluse alisema kuwa kuna umuhimu wa
wakulima kuweza kutumia teknolijia ya umwagiliaji kwa njia ya matone ya maji
ili kuweza kutunza na kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi mengine ya
kibinadamu, hivyo kuweza kuokoa gharama kwa mkulima.
Maonyesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi Nanenane nchini yalisimama kufanyika kwa mwaka jana wa 2021 kutokana na serikali kufanya tathimini ya maonyesho hayo ambayo kwa sasa yanasimamiwa na Serikali.
No comments:
Post a Comment