Breaking News

May 2, 2022

WAZIRI PINDI AHIMIZA TAWA KUTUMIA FURSA YA FILAMU YA ROYAL TOUR KATIKA UWEKEZAJI

 WAZIRI PINDI AHIMIZA TAWA KUTUMIA FURSA YA FILAMU YA ROYAL TOUR KATIKA UWEKEZAJI

Na Lilian Lucas,Morogoro                                                                                        

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa menejimenti ya TAWA kuandaa mazingira ya uwekezaji kupitia filamu ya Royal Tour iliyozinduliwa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na fursa za kiuchumi zitakazopatikana.

Waziri Chana alisema hayo jana kwenye ziara yake ya kikazi katika ofisi ya TAWA iliyopo Morogoro na kuongeza  na uongozi  na menejimenti ya TAWA ikiwa mwenelezo wa ukaguzi wa maeneo ya uwezekezaji katika sekta ya utalii zilizopo katika Wizara yake.

Alisema Royal Tour ni filamu inayotangaza vivutio vilivyopo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vivutio vilivyopo hapa nchini ni vingi ikiwemo  mapori ya akiba 27,hifadhi 22,vukwe (beach) kilometa 1400,Mapori yanayomilikiwa na vijiji (WMA) 30. Kwamba uwepo wa vivutio hivyo iwapo hazitaweza kuvienzi,kutunza, havitalinda kwa vizazi vya sasa na baadae itakuwa kazi bure.

Alisema filamu ya Royal Tour iliyandaliwa na Rais Samia inayonesha ya kuwa Tanzania ni sehemu salama ya utalii na uwekezaji,kwamba TAWA ndiyo Taasisi yenye dhamana ya kusimamia uwekezaji katika maeneo ya hifadhi.

Ameipongeza TAWA kutenga maeneo ya uwekezaji kwenye hifadhi ili kuweza kuongeza pato na ajira kwa watu wanaoishi katika maeneo hayo.

Wizara ya Maliasili na utalii wamejipanga kupita TANAPA,TAWA,maeneo ya malikale na maeneo mengine ya utalii.

Alisema utalii unachangia pato la taifa kwa  asilimia 17 huku ikitoa ajira 1500,ajira za moja kwa moja na ajira zisizo za moja kwa moja,hivyo ni jukumu la kila taasisi kutimiza wajibu kwa katika kuhakikisha pato la taifa linalotokana na sekta ya utalii linaongezeka kutoka pato lililopo sasa.

Alisema utalii linaanzia wageni wanapoingia kwa kuzingatia itifaki kwa kuzingatia uwekezaji katika sekta ya usafiri,chakula cha asili kwa watalii,kubadilisha fedha za kideni ambapo taasisi za kifedha zijiandae vizuri kuwahudumia wageni watakohitaji huduma hiyo.

Alielezea faida za ujio wa watalii itasaidia kupaua wigo kwa wananchi na taasisi jinsi ya kutumia vifaa vya asili vilivyopo kwa manufaa zaidi ya  uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Waziri Chana upo kwenye ziara maalum katika kuhagua maeneo ya uwekezaji yaliandaliwa na TAWA ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan  ambapo amejipambanua uinua sekta ya utalii kupitia filamu ya Royal Tour.

No comments:

Post a Comment