Breaking News

Jan 16, 2022

MWANANCHI MWENYE ULEMAVU AOMBA BAJAJI KWA RAIS SAMIA


                        JUMA RAMADHAN MKAZI WA TUNGI MANISPAA YA MOROGORO

Mwananchi mwenye ulemavu aomba bajaji kwa Rais Samia

Na.Thadei Hafigwa,Morogoro

MKAZI mmoja wa kata ya Tungi,Manispaa ya Morogoro Juma Ramadhan(58) mwenye ulemavu wa viongo(pichani) amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano,Samia Suluhu Hassan ampatie chombo cha usafiri aina ya bajaji atakayotumia kumrahisishia katika shughuli zake za kiuchumi.

Ramadhan mwenye namba ya simu 0686989841 alitoa ombi hilo kwa Rais Samia jana mjini Morogoro wakati akiongea na waandishi wa habari kuelezea kilio chake huku akielezea changamoto alizopata siku za nyuma kutoka kwa askari mgambo wa manispaa waliokuwa wakiendesha uperesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo kufanya biashara kandokando ya barabara.

Alidai yeye alikuwa ni miongoni mwa wahanga wa zoezi hilo ambapo avunjiwa meza yake aliyokuwa akiitumia kuuza matunda na mihogo huku fedha alizokuwaliovunja meza yake na kupoteza

“Ninamuomba Mheshimiwa Rais Samia anisaidie kupata bajaji ili inisaidie katika shughuli zangu za kiuchumi niondokane na adha ya kuombaomba maana mtaji wangu umepotea wakati wa uperesheni ya kuondoa wafanyabiashara wadogowadogo”alisema

Aidha,Ramadhan alisema kuwa kwa kipindi kirefu alikuwa akijihusisha biashara ya ndogondogo kuuza matunda mbele ya msikiti kuu uliopo kandokando ya barabara ya boma kabla ya kuvunjiwa meza na mgambo,kwa sasa hana shughuli anayofanya zaidi ya kuomba wahisani ili kutunza familia yake ya watoto watano.

Anasema kuwa ana imani kubwa ya Rais Samia kuwa atasikia kilio chake kutokana na upendo na huruma aliyokuwa nayo kwa watu wanyonge na wenye mahitaji maalum.

Pia,alisema kuwa kama ya kuvunjiwa meza yake ya biashara aliwahi kujiwekea akiba na kumwezesha kujifunza udereva wa bajaji na kufanikiwa kukata leseni katika mamlaka husika,ambapo alikuwa na ndoto siku moja amiliki bajaji.

No comments:

Post a Comment